YANGA imejiandaa kwa penalti katika mchezo wa leo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini bado imeonyesha udhaifu katika kupiga na hata kupangua mikwaju hiyo ya penati.
Zoezi hilo liliendelea wakati watu mbalimbali wenyeji wa hapa wakizunguka kwenye uwanja wa Zamalek waliokuwa wakifanyia mazoezi Yanga wakidai kuwa walikuwa wakifanya shughuli za ulinzi na kuweka mambo sawa ingawa kocha Kostadin Papic alikosa amani akawa anawahamisha wachezaji wake nusu uwanja kila mara.
Ingawa wanachama wa Yanga waliokuwapo katika mazoezi ya juzi jioni kwenye Uwanja wa Zamalek walidai kwamba ni kutokana na baridi, lakini kosakosa na utendaji wa makipa haukuvutia.
Wachezaji wengine walikuwa wakipaisha au kupiga nje na hata walipopiga ndani ya goli makipa Shabaan Kado na Said Mohammed bado walikuwa kwenye wakati mgumu na hawakupangua hali ambayo imezua hofu kwa mustakabali wa Yanga endapo wakitoka sare leo.
Yanga na Zamalek zilipokutana katika mechi ya awali zilitoka sare ya na kama leo ikipata sare ya 2-2 italazimika kujiandaa na mikwaju ya penati itakayoamua mshindi.
Lakini Zamalek ambao Uwanja wao una huduma zote kwa timu za vijana wenye umri mbalimbali mpaka wakubwa, imejiandaa kumaliza mchezo ndani ya dakika 90 huku kocha Hassan Shehata akitamba kuwa Mido yupo fiti licha ya kwamba Zaki hayupo.
Mechi hiyo itachezwa usiku kuanzia saa 12.00 za hapa sawa na saa moja kamili nchini Tanzania katika muda ambao huwa na upepo mkali sambamba na baridi ambayo huumiza mifupa.
HABARI ZOTE ZA CAIRO KWA HISANI YA MICHAEL MOMBURI WA MWANASPOTI

.png)
0 comments:
Post a Comment