• HABARI MPYA

  Saturday, September 07, 2019

  SIMBA SC YAAJIRI MTENDAJI MKUU MPYA KUTOKA AFRIKA KUSINI, ANACHUKUA NAFASI YA MAGORI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba ya Dar es Salaam imemtambulisha raia wa Afrika Kusini, Senzo Mazingisa kuwa Mtendaji wake Mkuu mpya akichukua nafasi ya Crescentius Magori aliyeamua kujiuzulu.
  Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam leo, Magori alimtambulisha Mazingisa na kumwagia sifa kwamba ana uzoefu ulioanzia kuongoza klabu kubwa kwao, Afrika Kusini.
  Alizitaja baadhi ya klabu ambazo Mazingisa amezitumikia katika nafasi mbalimbali za utendaji ni pamoja na Platinum Stars, Orlando Pirates na Shirikisho la Soka Afrika Kusini (SAFA).

  Crescentius Magori (kulia) akimkaribisha Mtendaji Mkuu mpya, Senzo Mazingisa leo hoteli ya Serena

  Kwa upande wake akizungumza baada ya kutambulishwa kwa Waandishi wa Habari, Mazingisa alisema amefurahi kujinga na Simba SC, kwani ni klabu kubwa Afrika.
  “Simba ni timu kubwa sana, nimekuwa naifatilia kwa muda sasa. Nimejifunza kuwa ni timu kubwa, na tunaweza kuifanya kuwa kubwa zaidi, sio tu ukanda wa Afrika Mashariki bali kuwa klabu kubwa zaidi Afrika,” alisema Mazingisa.
  Simba SC ambayo ipo chini ya bilionea, Mohamed ‘Mo’ Dewji kwa sasa inakuwa klabu nyingine nchini baada ya Azam FC na Yanga SC kuajiri Watendaji wa kigeni, ambao hata hivyo hawakudumu. 
  Yanga SC ikiwa chini ya bilionea, Yussuf Manji ilimuajniri Mkenya Patrick Naggi mwaka 2013, lakini aliondoka baada ya kupingwa na wanachama waliotaka mchezaji wa zamani wa klabu huyo, Lawrence Mwalusako aendelee na majukumu hayo, wakati Azam FC iliajiri Muingereza mwenye asili ya Uganda Eligius Elibankya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAAJIRI MTENDAJI MKUU MPYA KUTOKA AFRIKA KUSINI, ANACHUKUA NAFASI YA MAGORI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top