• HABARI MPYA

  Wednesday, March 15, 2017

  YANGA WAIFUATA ZANACO KESHO BILA NGOMA, TAMBWE

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  WASHAMBULIAJI wote tegemeo wa Yanga, Mrundi Amissi Joselyn Tambwe na Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma hawatasafiri na timu kesho kwenda Zambia kwa mchezo wa marudiano na wenyeji, Zanaco hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Tambwe hakucheza kabisa mechi ya kwanza dhidi ya Zanaco Jumamosi ya Machi 11, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Ngoma alijitonesha goti katika mchezo huo baada ya kurejea kufuatia kuwa nje tangu Janauri.
  Katibu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba pamoja na wawili hao ambao ni majeruhi, pia klabu itawakosa kipa Beno Kakolanya, beki Pato Ngonyani, kiungo Yussuf Mhilu na washambuliaji wengine wawili, wote wazawa, Malimi Busungu na Matheo Anthony ambao pia ni wagonjwa. 
  Donald Ngoma akiugulia maumivu baada ya kujitonesha goti katika mchezo wa kwanza dhidi ya Zanaco Jumamosi

  Mkwasa amesema wachezaji 20 tu ndiyo watasafari na timu kesho kwa ndege ya Shirika la Kenya kwenda Lusaka kwa ajili ya mchezo huo wa Jumamosi na kwa bahati mbaya hakutakuwa na mshambuliaji halisi hata mmoja.
  Hao ni makipa; Deogratius Munishi ‘Dida’ na Ally Mustafa ‘Barthez’, mabeki ni Oscar Joshua, Mwinyi Hajji Mngwali, Hassan Kessy, Juma Abdul, Vincent Bossou, Andrew Vincent ‘Dante’, Kevin Yondan na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
  Viungo ni Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Justine Zulu, Said Juma ‘Makapu’, Juma Mahadhi, Simon Msuva, Geoffrey Mwashiuya, Obrey Chirwa na Emanuel Martin. 
  Yanga inahitaji ushindi wa ugenini Jumamosi ili kwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA WAIFUATA ZANACO KESHO BILA NGOMA, TAMBWE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top