• HABARI MPYA

    Wednesday, March 15, 2017

    TRA YAWAFUNGIA NJE MAOFISA WA TFF, SOKA YA TANZANIA KIZANI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imezifunga ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na deni kubwa la kodi na la muda mrefu.
    Zoezi hilo limefanyika mchana wa leo chini ya Kampuni ya Udalali na Minada ya Yono, ambayo kwa sasa ndiyo inazishikilia ofisi hizo baada ua kuwatoa nje wafanyakazi wote wa TFF na kuwataka waache kila kitu ndani.
    Hakuna Ofisa wa TRA aliyekuwa tayari kuzungumza haraka wakati wa zoezi hilo leo mchana, lakini habari zinasema ni madeni ya tangu uongozi uliopita, chini ya Rais Leodegar Tenga kabla ya uongozi wa sasa, chini ya Rais Jamal Malinzi.
    Na deni kubwa zaidi linatokana na kodi za mishahara ya aliyekuwa kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Mbrazil Maximo kwa miaka minne tangu 2016 hadi 2010.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema msafara wa Tanzania unaokwenda kwenye uchaguzi wa CAF utageuza kesho

    Deni lingine linalosababisha ofisi za TFF kufungwa ni la kodi ya Ongezeko la Thamani (VaT) la ziara ya timu ya taifa ya Brazil nchini mwaka 2010 ilipokuwa njiani kwenye Afrika Kusini kwenye fainali za Kombe la Dunia.
    Alipotafutwa Rais wa TFF, Jamal⁠ Malinzi alisema; “Ni kweli nasikia hilo limetokea na ni kwa sababu ya madeni ya kodi za mishahara ya ⁠⁠⁠Maximo na VaT ya mechi ya Brazil,”.
    Malinzi akaongeza kwamba kutokana na tatizo hilo, msafara wa Tanzania uliopo kwenye mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Shirikisho la Soka (CAF) mjini Addis Ababa itabidi kesho urudi Tanzania.
    Ofisa wa Yono akiwa kwenye geti kuu la kuingia ofisi za TFF Uwanja w Karume baada ya kufunga
    Haiingii mtu tena ndani, maana yake hata mazoezi ya Serengeti Boys yanasimama

    “Msafara wa Tanzania uko Addis Ababa na kesho ni uchaguzi mkuu CAF na pia itapigwa kura ya Zanzibar kupewa uanachama wa CAF na Tenga kuingia FIFA, msafara inabidi urudi na kuacha yote haya,”amesema Malinzi. 
    Pamoja na haya, suala hili litaathiri mambo mengi ikiwemo maandalizi ya timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kwa ajili ya fainali za Afrika nchini Gabon Mei mwaka huu.
    Na si ajabu operesheni zote za soka ya Tanzania zikasimama kwa muda iwapo TRA itaendelea kuzifungia ofisi za TFF.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TRA YAWAFUNGIA NJE MAOFISA WA TFF, SOKA YA TANZANIA KIZANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top