• HABARI MPYA

  Monday, March 13, 2017

  MALAWI YAJITOA KUFUZU CHAN NA AFCON SABABU 'WAMEFULIA'

  CHAMA cha Soka Malawi (FAM) kimeamua kujitoa kwenye mechi za kufuzu za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) na Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) kutokana na matatizo ya kifedha.
  Kwa mujibu wa taarifa ya FAM na kusainiwa na Mtendaji Mkuu wa chama, Alex Gift Gunda, uamuzi huo umefikiwa Jumapili katika kikao cha Kamati ya Utendaji.
  "Chama cha Soka Malawi (FAM) kinapenda kuutaarifu uma na wadau wake wote kwamba kikao chake cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika mjini Lilongwe Machi 11, 2017, chama, pamoja na mambo mengine, kilijadili uteuzi wa kocha wa timu ya taifa ya wakubwa na hali ya kifedha ya timu ya taifa ya Malawi,"imesema taarifa hiyo.
  FAM imepanga kuwekeza nguvu zaidi kwenye soka ya vijana ili kuwa na vikosi imara vya timu za taifa za vijana chini ya umri wa miaka 15, 17 na 20. 
  matarajio ya ni baadaye kuwa na timu bora na ya ushindani ya taifa kutokana na timu hizo za vijana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MALAWI YAJITOA KUFUZU CHAN NA AFCON SABABU 'WAMEFULIA' Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top