• HABARI MPYA

  Friday, April 07, 2023

  TIMU ZA TAIFA NDONDI WANAWAKE NA WANAUME ZATEULIWA


  SHIRIKISHO la ngumi Tanzania (BFT) Aprili 5 lilifanya mashindano ya mchujo na kupata mabondia watakao wakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya kanda ya tatu Afrika yatakayofanyika uwanja wa ndani wa taifa (indoor stadium) tarehe 18-22 Aprili 2023. 
  Kwa mujibu wa Makore Mashaga, Katibu Mkuu Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), mashindano hayo yatashirikisha nchi 14 wanachama wa kanda ya tatu.
  Amesema mchujo huo umefanyika katika ukumbi wa mazoezi wa timu ya ngumi ya JKT Mgulani. Jumla ya mabondia 22, ikiwa wanaume 16 na wanawake 6 ndio waliochagulia miongoni mwa mabondia 56 walikuwa katika maandalizi ya mashindano hayo.
  Amesema mabondia waliochaguliwa ni wale walionyesha uwezo mzuri kuwashinda wenzao kutoka katika kambi tatu tofauti zilizokuwa zikiendelea na mazoezi ya kujiandaa na mashindano hayo kutoka katika kambi za timu ya ngumi ya Ngome, timu ya ngumi ya Magereza na timu ya ngumi ya JKT Mgulani.
  Mashaga amesema kwa sasa mabondia waliochaguliwa watafanya mazoezi katika kituo kimoja JKT Mgulani.
  Ameongeza kwamba Kamati ya BFT imechagua kituo hicho kutokana na kuwepo kwa miundo mbinu mizuri ya kuwezesha kufanya mazoezi ya ngumi kwa ufanisi kwa maandalizi ya mwisho na ya pamoja.
  Amesema nchi zitakazoshiriki mashindano hayo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Ethiopia, Somalia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kongo Brazzaville, Afrika ya Kati, Gabon, Cameroon na Equatorial Guinea.
  Aidha, Mashaga amewataha mabondia waliochaguliwa kuunda timu za taifa za Tanzania kwa wanaume, wanawake, Makocha na kamati ya ufundi pia kwa ajili ya mashindano hayo.
  ORODHA YA MABONDIA WA KIUME WALIOCHAGULIWA TIMU YA TAIFA
  Karim Juma - Minimume
  Yohana Keneth - Fly
  Abdalah Salum - Bantam
  Hassan Waziri - Feather
  Rashid Mrema - Light
  Alex Isendi - Light Welterweight
  Mohamed Swalahe - Light Welter
  Atanas Ndiganya - Welter
  Joseph Phillip - Light Middle
  David Chanzi - Middle
  Joshua Shadrack - Middle
  Alphonce Abel - Middle
  Yusuf Changalawe - Light Heavy
  Nizza Abdalahamani - Light Heavy
  Jofrey Peter - Cruser
  Alex Sitta - Super Heavy
  ORODHA YA MABONDIA WA KIKE WALIOCHAGULIWA TIMU YA TAIFA
  Rahma - Minimum
  Mariam Richard - Light Flyw
  Shakila Abdalah - Fly
  Aisha Iddi - Bantam
  Leila Yazidu - Bantam
  Beatrice Ambrose - Light
  MAKOCHA
  1. Samwel Batman – (IBA 1 Star)
  2. Hassan Mzonge
  3. Mussini Mohamed
  4. Rogata Damian (IBA 1 Star)
  5. Undule Lang’son
  6. Haji Abdalah
  KAMATI YA UFUNDI
  1. Michael Changarawe – Mwanza
  2. Robert Sululu – Dar es salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIMU ZA TAIFA NDONDI WANAWAKE NA WANAUME ZATEULIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top