• HABARI MPYA

  Wednesday, April 05, 2023

  MWAMEJA ALIPOIONGOZA SIMBA SC KUTINGA FAINALI KOMBE LA CAF 1993


  NAHODHA wa Simba SC, Mwameja Mohamed akiwaongoza wachezaji wenzake wa Simba SC kuingia Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru) Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la CAF dhidi ya 
  AS Aviação ya Angola mwaka 1993. Simba ilishinda 3-1 na mchezo wa ugenini ilitoa sare ya 0-0 hivyo kwenda Fainali ambako ilifungwa 2-0 na Stella Club d'Adjamé ya Ivory Coast hapo hapo Uhuru baada ya sare ya 0-0 Abidjan.
  Novemba 27, mwaka 1993 dhidi ya
  Stella, maarufu kama Stella Abidjan waliibuka na ushindi wa 2-0, mabao ya Kouame Desré Kouakou dakika ya 18 na N'guessan Serges dakika ya 77. Mechi ya kwanza Novemba 14 timu hizo zilitoka sare ya 0-0 Jijini Abidjan, Ivory Coast.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWAMEJA ALIPOIONGOZA SIMBA SC KUTINGA FAINALI KOMBE LA CAF 1993 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top