• HABARI MPYA

  Saturday, October 01, 2022

  IBRA CLASS AMDUNDA MMEXICO KWA KNOCKOUT


  BONDIA Ibrahim Mgender 'Ibrah Class' usiku wa jana amefanikiwa kumshinda mpinzani wake, Gustavo Pina Melgar  ‘Alan Pina’ wa Mexico kwa Knockout (KO) raundi ya tisa uzito wa Super Feather ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
  Mabondia wengine wa Tanzania walishinda kwa pointi, Juma Choki dhidi ya Jose Hernandez Rizo wa Mexico uzito wa Super Feather, Emmanuel Mwakyembe dhidi ya Mkenya, Nicolaus Mwangi uzito wa Light na Adam Mrisho dhidi ya Sameer A. Pandya wa Kenya uzito wa Super Light.
  Mambo hayakuwa mazuri kwa Mwinyi Mzengela aliyedundwa kwa Knockout (KO) na Sabari J wa India.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IBRA CLASS AMDUNDA MMEXICO KWA KNOCKOUT Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top