• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 08, 2020

  MESSI ATOKEA BENCHI NA KUPIGA MBILI BARCA YASHINDA 5-2


  Nahodha Lionel Messi (kulia) akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Barcelona dakika ya 61 kwa penalti na 82 kufuatia kutokea benchi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ansu Fati katika ushindi wa 5-2 dhidi ya Real Betis kwenye mchezo wa La Liga usiku wa jana Uwanja wa Camp Nou. Mabao mengine ya Barcelona yalifungwa na Ousmane Dembele dakika ya 22, Antoine Griezmann dakika ya 49, ambaye awali alikosa penalti dakika ya 33 na Pedri dakika ya 90. Mabao ya Real Betis iliyomaliza pungufu baada ya A. Mandi kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 60 baada ya kuonyeshwa njano ya pili yalifungwa na Arnaldo Sanabria dakika ya 45 na ushei na Loren Moron dakika ya 73
   

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI ATOKEA BENCHI NA KUPIGA MBILI BARCA YASHINDA 5-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top