• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 04, 2019

  AUSSEMS AMETUKUMBUSHA YA MAREHEMU JAMES SIANG'A SIMBA

  Na Mustafa Mtupa, DAR ES SALAAM
  Nilikuwa bado mdogo saana kipindi ambacho mkenya James Agrey Siang'a anakinoa  miongoni mwa vikosi Bora kuwahi kutokea kunako klabu ya Simba.
  Mahaba yangu na mchezo huu yalinifanya nitake kujua na kuanza. Hata kudadisi na kuyajua yaliyojiri kwa wakati huo.
  Ni wakati huo ambapo simba ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Klabu bingwa barani Afrika.
  Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems amefukuzwa Simba SC licha ya kuifikisha klabu Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika

  Ni wakati huo ambapo mchaga wa kwanza kucheza mpira Christopher Alex alipokuwa kwenye ubora wake.
  Ni wakati huu wa simba ya kina watukutu kama  Goerge  masatu. Chini ya kocha James ambaye alikuwa kama mchawi wa mpira. 
  Babu aliniambia kwamba simba hii ilikuwa moto wa kuotea mbali na yanga kila alipokuwa anatokeza.alikuwa anapotea vibaya.na hata timu nyengine zilikuwa zinaanza kufungwa kabla hata ya kuingia uwanjani kwa hofu tu.
  Lakini hadithi hii nzuri na ya kusisimua ilikuja kugeuka ya kutisha na ya kutia huruma pale mkenya huyu alipofungashiwa virago na kurudishwa kwao kenya.
  Wakasahau hata zile nyakati za furaha na faraja walizowahi kuwa nazo walipokuwa na mchawi huyu wa soka.
  Kilicho mkuta Patrick ambaye wanasimba walibatiza jina la (Professor)  hakina tofauti na kile kilicho mkuta marehemu  Siang'a.
  Ni makocha wawili ambao wamefanana mwisho wao.mwisho ambao umeacha  maswali lukuki namna ambavyo wametimuliwa.
  Kocha Mkenya, marehemu James Siang'a aliiongoza Simba SC kwa mafanikio pia kati ya 2001 na 2003

  Nilipomuuliza Babu kwanini Siang' a aliondoka?  Wala hakupepesa macho akaniambia ni mfumo tu.
  Patrick hakika amecha alama isiyo futika daima kwa kile ambacho amekiacha lakini kulikuwa kuna kitu kikubwa zaidi ya kile ambacho amekionesha ambacho ni mfumo.
  Hawa makocha wawili wali wasahaulisha  wanasimba maumivu ya uchungu wa mpira katika nyakati zoote walizokuwa wanahudumu lakini mwisho wao umekuwa wa kashfa na fedheha.
  Mungu akupunguzie adhabu ya kaburi mchawi wa mpira James Agrey Siang' a na nakutakia maisha mema Patrick hakika jina lako limeandikwa.
  (Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa namba +255 687 058 966 au @mtotoWamkulima99 kwenye instagram)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AUSSEMS AMETUKUMBUSHA YA MAREHEMU JAMES SIANG'A SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top