• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 04, 2019

  SAMATTA AFUNGA PENALTI LAKINI KRC GENK YATUPWA NJE KWA MATUTA KOMBE LA UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amefunga penalti lakini timu yake, KRC Genk imetupwa nje ya michuano ya Bora Kombe la Ubelgiji baada ya kufungwa kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 3-3 na Royal Antwerp katika mchezo wa hatua ya 16 Bora Uwanja wa Bosuilstadion mjini Deurne.
  Huo ni mwendelezo wa matokeo mabaya mno kwa Genk wakifikisha mechi nane bila kushinda, wakifungwa ya sita huku nyingine mbiki wakitoa sare – baada ya kushinda mara ya mwisho Oktoba 26 dhidi ya Cercle Brugge 1-0.
  Katika sare ya 3-3 mabao ya Genk yalifungwa na Joakim Maehle dakika ya nne, Wesley Hoedt aliyejifunga dakika ya 81 na  Junya Ito dakika ya 105 na ushei na ya Royal Antwerp yamefungwa na Simen Juklerod dakika ya 30 na Dieumerci Mbokani mawili dakika ya 72 na 104.

  Samatta jana amecheza mechi ya 178 akiwa amefunga mabao 71 katika katika mashindano yote tangu ajiunge na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Katika ligi ya Ubelgiji pekee amecheza mechi 138 akiwa amefunga mabao 54, kwenye Kombe la Ubelgiji amecheza mechi 10 sasa na kufunga mabao mawili, katika Super Cup mechi moja, Ligi ya Mabingwa Ulaya mabao matau, mechi nne.
  Kikosi cha Genk kilikuwa: Vandevoordt, Maehle, Dewaest, Lucumí, Borges/De Norre dk108, Cuesta/Wouters dk81, Berge, Ndongala, Hrosovsky/Bongonda dk75, Paintsil/Ito dk68 na Samatta.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA AFUNGA PENALTI LAKINI KRC GENK YATUPWA NJE KWA MATUTA KOMBE LA UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top