• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 20, 2017

  TOTO AFRICANS YASONGA MBELE KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION

  Na Abdallah Chaus, MWANZA 
  TIMU ya Toto Africans ya Mwanza imefuzu hatua ya 32 Bora ya Kombe la Azam Sports Federation Cup baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Eleven Star ya Kagera jioni ya leo Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
  Katika mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki wachache, Toto Africans walijipatia mabao yao kupitia kwa washambuliaji wake Bernard Isidory dakika ya tatu na Yusuph Khamis dakika ya 64. 
  Khamis alifunga baada kuingia katika kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Isidory, wakati bao la Eleven Star lilifungwa na Nassor Kimera dakika ya 43.
  Wachezaji wa Toto Africans wakishangilia bao lao la ushindi leo Nyamagana

  Michuano ya Azam Sports Federation Cup inatarajiwa kuendelea kesho ksa Mshikamano ya Dar es Salaam kucheza na Polisi Tanzania ya Morogoro; Rhino ya Tabora na Alliance ya Mwanza; Majimaji Rangeres ya Lindi itapambana na Mbeya Kwanza ya Mbeya; Njombe Mji na Mji Mkuu ya Dodoma; Ashanti na Friends Rangers za Dar es Salaam; Kagera Sugar na Makambako wakati Stand United ya Shinyanga itacheza na AFC ya Arusha.
  Desemba 22, mwaka huu kutakuwa na mechi za Green Warriors na Simba; Polisi Dar itapambana na Mgambo JKT ya Tanga; Kariakoo ya Lindi na Transit Camp ya Dar ila kwa sasa imeweka maskani Shinyanga; Biashara ya Mara itacheza na Mawenzi Market ya Morogoro; Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani itacheza na Madini FC ya jijini Arusha huku Mufindi United na Pamba ya Mwanza ilihali Singida United itacheza na Bodaboda FC.
  Mchezo kati ya Simba na Green Warriors utaochezwa Desemba 22, utakuwa ni maalumu kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa michuano hiyo msimu. Sababu Simba ndiye bingwa mtetezi.
  Siku ya Desemba 23, mwaka huu Azam FC itacheza na Area C; African Lyon ya Dar es Salaam na Kiluvya United ya Pwani; Makanyagio itapambana na Mbao; Mwadui na Pepsi; Majimaji na New Generation wakati Mbeya City itacheza na Ihefu.
  Desemba 24, 2017 Yanga SC itacheza na Reha FC; Burkina ya Morogoro na Lipuli ya Iringa;  Coastal Union ya Tanga na Dodoma Fc ya Dodoma; Shupavu na Real Mojamoja wakati Villa Squad itacheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TOTO AFRICANS YASONGA MBELE KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top