• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 30, 2017

  WANACHAMA YANGA MWANZA WAJITOLEA KUSAJILI WACHEZAJI 10

  Na Abdallah Chaus, MWANZA 
  WANACHAMA wa matawi ya Yanga mkoani Mwanza wamekutana katika mkutano wao wa mwisho wa mwaka wenye lengo la kujadili mustakabali na mwenendo klabu yao katika msimu huu.
  Katika mkutano huo uliohudhuriwa na Kaimu Mwenyekiti wa Yanga,  Clement Sanga wanachama hao kupitia kwa Mwenyekiti wa Matawi hayo, Salehe Akida wamedhamiria kufanya harambee katika matawi yote ya Mkoa wa mwanza ili kuhakikisha wanapata fedha za kuwawezesha kusajili wachezaji 10 katika msimu ujao kama nia na lengo la kuweza kua karibu na timu yao.
  "Hakika tumedhamiria kufanya makubwa katika msimu ujao kwa kuweza kuyafanya matawi yetu ya wanachama wa Mwanza kuwa yakuigwa na kuwa mfano katika matawi yote Tanzania".

  katika hatua nyingine wanachama hao wanechangishana fedha tasilimu shilingi laki tisa na elfu thelathini kwa lengo la kuwapa motisha wachezaji kuweza kujituma katika mchezo wao wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mbao FC utaokaochezwa siku ya jumapili kwenye uwanja wa ccm kirumba mwanza majira ya saa kumi kamili jioni
  Akizungumza katika mkutano huo makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga Amewashukuru wanachama hao kwa umoja wao wanaouonesha katika kuinga mkono timu yao kwa kusafiri kwenda kuipa hamasa na kuwataka watulie ili waweze kuutetea ubingwa wao msimu huu
  ""Yanga ni taasisi kubwa na inawanachama Tanzania Nzima wote nia yetu ni kuhakikisha yanga inasonga mbele na asitokee mtu yeyote kutuvuruga na akitokea mtu huyo basi tumchukulie hatua mara moja ili kuiboresha yanga yetu"""
  huu ni mkutano wao wa nne baada ya mikutano mitatu iliyofanyika mwaka huu katika Mkoa wa Mwanza ambao ni desturi yao kwajili ya kuharishana kinachoendelea katika kila matawi
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WANACHAMA YANGA MWANZA WAJITOLEA KUSAJILI WACHEZAJI 10 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top