• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 22, 2017

  RAIS KARIA ‘AWAITA FARAGHA’ WAHARIRI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia atakutana na Wahariri wa Habari za Michezo Jumatano wiki ijayo, Desemba 27,2017.
  Taarifa Ofisa Habari Msaidizi wa TFF, Clifford Ndimbo imesema kwamba pamoja na mambo mengine, Rais Karia atazungumzia miezi yake minne tangu aingie madarakani pamoja na vitu vilivyofanyika katika muda huo.
  Aidha Rais Karia ataelezea changamoto mbalimbali zilizopo TFF pamoja na njia  zinazotumika, zitakazotumika kuweza kupiga hatua kwa mpira wa Tanzania.
  Hata hivyo, taarifa hiyo haikutaja Wahariri walioalikwa wala sehemu na muda ambao Rais Karia atafanyia mkutanio wake wa kwanza kwa ujumla kuzungumza na vyombo vya Habari za Michezo tangu aingie Karume Agosti 12, mwaka huu baada ya uchaguzi uliofanyika mkoani Dodoma.
  Wallace Karia (wa pili kulia) akiwa na Makamu wake, Michael Wambura (kulia) wakifurahia ushindi wa Simba wa Ngao ya Jamii Agosti 23, mwaka huu 
  Makamu wa Rais wa TFF ni Michael Wambura na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Lameck Nyambaya wa Dar es Salaam, Khalid Abdallah wa Tanga, Francis Ndulane wa Pwani na Morogoro, Mohamed Aden wa Singida na Dodoma, Dunstan Mkundi wa Lindi na Mtwara na James Mhagama wa Njombe la Ruvuma.
  WEngine ni Elias Mwanjala wa Mbeya na Iringa, Kenneth Pesambili wa Katavi na Rukwa, Issa Bukuku wa Kigoma na Tabora, Sarah Chao wa Arusha na Manyara, Mbasha Matutu wa Shinyanga na Simiyu, Vedastus Lufano wa Mara na Mwanza na Salum Chama wa Kagera na Geita.
  Na Karia anakutana na Wahariri wa Habari baada ya mwanzo mbaya TFF, ikishuhudiwa soka la Tanzania likizidi kuporomoka kwa kasi, Ligi Kuu ikiwa inaahirishwa mara kwa mara, shughuli za kiutawala ofisni Karume zinakwenda ovyo, ikiwemo masuala ya usajili.
  Na mwezi huu timu ya Bara imevunja rekodi ya kufanya vibaya kwenye michuano ya CECAFA Challenge baada ya kushika nafasi ya mwisho – na kwa ujumla Watanzania wamekwishaanza kupoteza imani na uongozi wake mapema tu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RAIS KARIA ‘AWAITA FARAGHA’ WAHARIRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top