• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 21, 2017

  MKAKATI WA KUTETEA UBINGWA; YANGA WAUNDA ‘KAMATI NZITO’ PEDEZYEE NDAMA, KATABARO NDANI

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KATIKA kuhakikisha wanatetea ubingwa wao Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC wameunda upya Kamati ya Mashindano itakayokuwa na watu 23.
  Taarifa ya Yanga kwa vyombo vya Habari jioni ya leo, imesema kwamba Kamati hiyo itakuwa chini ya Mwenyekiti Hussein Nyika, Makamu wake Mustapha Ulungo na Katibu Mkuu, Samuel Lukumay.
  Wajumbe wa Kamati hiyo ni Ndama Shaaban Hussein maarufu kama 'Pedezyee Ndama Mtoto wa Ng'ombe', Omary Chuma, Majjid Suleiman, Mussa Katabaro, Yusuphed Mhandeni, Beda Tindwa, Jackson Maagi, Lameck Nyambaya, Nicko Meela, Edward Urio, Rodgers Gumbo, Edgar Mutani, Shijja Richard, Sanga Kayanda, Hamad Islam, Paschal Kihanga, Isihaka Sengo, Bahati Mwaseba, Rashid Msinde, Khalfan Kigwelembe, Yanga Makanga, Rodgers Lemlembe na Leonard Chigango.
  Ndama Shaaban Hussein maarufu kama 'Pedezyee Ndama Mtoto wa Ng'ombe' yumo kwenye Kamati ya Mashindano ya Yanga

  Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Habari wa Yanga, Dissmas Ten uteuzi huo umefanyika leo katika kikao cha Kamati ya Utendaji makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam.
  Kwa sasa Yanga inakamata nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu kwa pointi zake 21 baada ya mechi 11, ikizidiwa pointi mbili na zote Simba na Azam zilizo juu yake.    
  Na baada ya mapumziko ya wiki tatu kupisha michuano ya CECAFA Challenge iliyomalizika Jumapili Kenya, Ligi Kuu itaendelea mwishoni mwa mwezi huu na Yanga watashuka dimbani Desemba 31 kumenyana na Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MKAKATI WA KUTETEA UBINGWA; YANGA WAUNDA ‘KAMATI NZITO’ PEDEZYEE NDAMA, KATABARO NDANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top