• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 27, 2017

  PAMBA WABEBA WAANDISHI WA HABARI MECHI NA BIASHARA MARA KWA KUMUHOFIA WAMBURA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Pamba FC ya Mwanza imejitolea kusafirisha Waandishi wa Habari kwenda Musoma mkoani Mara katika mchezo wao wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Biashara FC Jumamosi.
  Ofisa Habari wa Pamba FC, Johnson James amesema katika taarifa yake leo kwamba wanawaomba Waandishi wa Habari za michezo walioko Mwanza ambao wangependa kuhudhuria mchezo huo wajiorodheshe kwenye ofisi zake zilizopo barabara ya Posta Jijini Mwanza kwa ajili ya safari hiyo.
  “Lengo la kuwaomba wanahabari kujiorodhesha kwa ajili ya kufika Musoma kuushuhudia mchezo huo ni kutokana na mchezo wenyewe kuwa mgumu na unaovuta hisia za watu, hivyo tunawaomba wanahabari za michezo ambao mnahitaji kwenda mjiorodheshe,”.
  Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura (kulia) ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa FAM 

  James amesema lengo ni ili ikitokea sheria 17 na taratibu za mchezo huo zikakiukwa waweze kuripoti bila upendeleo aidha kwa Pamba au Biashara FC.
  James amesema kwamba pamoja na Makamu wa Rais wa  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura ndiye Mwenyekiti pia wa Chama cha Soka Mara (FAM) pia, lakini ni muumini wa sheria za soka hivyo hatarajii haki kutotendeka katika mchezo huo, ili mshindi apatikane kwa uhalali ndani ya dakika 90 za mchezo huo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PAMBA WABEBA WAANDISHI WA HABARI MECHI NA BIASHARA MARA KWA KUMUHOFIA WAMBURA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top