• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 29, 2017

  YUSSUF BAKHRESA AINGIZWA TUZO ZA VIJANA WENYE USHAWISHI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MMOJA wa Wakurugenzi wa Azam FC, Yusuf Bakhresa, amechaguliwa kugombea tuzo za vijana wenye ushawishi hapa nchini (Most Influential Young Tanzanian) zinazoandaliwa na Kampuni ya Avance Media.
  Yusuf amewekwa kwenye kipengele namba moja cha Wafanyabiashara (Business) kupitia Kampuni anayoiongoza ya Azam Media Ltd akiwa kama Mkurugenzi Mkuu.
  Kipengele hicho kinawahusu wafanyabiashara ambao wanaongoza makampuni kwa mafanikio hapa nchini, ambayo yanaipa thamani jamii katika nyanja za kijamii, kiuchumi na kiutamaduni na kuchangia kuunda picha nzuri ya bara la Afrika.
  Yusuf Bakhresa amekuwa akiwasaidia vijana mbalimbali wakiwemo wanasoka 

  Unaweza kumpigia kura Yusuf Bakhresa, ambaye amekuwa pia msaada mzuri wa kulea vipaji mbalimbali vya wanasoka nchini na kuwatafutia soko nje ya nchi, kwa kufuata taratibu zifuatazo;
  Hatua ya Kwanza: Fungua ukurasa wa tovuti hii ‘http://tz.avancemedia.org/’
  Hatua ya Pili: Ingia kwenye kipengele cha 'Business (in partnership with tanoebusiness.com)'
  Hatua ya Tatu: Chagua jina la 'Yusuf Bakhresa (Azam Media Ltd)
  Hatua ya Nne: Shuka mpaka chini, utakutana na sehemu ya kujaza jina lako, email yako, namba ya simu (including country code). Kisha bonyeza kitufe cha 'VOTE'.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YUSSUF BAKHRESA AINGIZWA TUZO ZA VIJANA WENYE USHAWISHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top