• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 22, 2017

  MNYAMA SIMBA AANZA KUTETEA TAJI LEO USIKU CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MABINGWA watetezi, Simba SC leo wanaanza kutetea taji la Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa kumenyana na Green Warriors, zote za Dar es Salaam katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, kuanzia Saa 1:00 usiku.
  Japokuwa michuano hiyo ilianza miezi miwili iliyopita, lakini mchezo huo ndio utakuwa maalumu kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa michuano hiyo msimu huu, kwa sababu Simba ndiyo wanaoshikilia taji baada ya kuwafunga Mbao FC 2-1 katika fainali Mei mwaka huu mjini Dodoma.
  Mechi nyingine za leo, Polisi ya Dar es Salaam itamenyana na Mgambo JKT ya Tanga; Kariakoo ya Lindi na Transit Camp ya Dar es Salaam, iliyohamishia maskani yake Shinyanga; Biashara ya Mara na Mawenzi Market ya Morogoro; Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani na Madini FC ya Arusha, Mufindi United na Pamba ya Mwanza na Singida United itacheza na Boda Boda FC.
  Michuano hiyo itaendelea Jumamosi na Azam FC watacheza na Area C; African Lyon ya Dar es Salaam na Kiluvya United ya Pwani; Makanyagio itapambana na Mbao; Mwadui na Pepsi; Majimaji na New Generation wakati Mbeya City itacheza na Ihefu.
  Jumapili, mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC watacheza na Reha FC; Burkina ya Morogoro na Lipuli ya Iringa;  Coastal Union ya Tanga na Dodoma Fc ya Dodoma; Shupavu na Real Mojamoja wakati Villa Squad itacheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MNYAMA SIMBA AANZA KUTETEA TAJI LEO USIKU CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top