• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 23, 2017

  MESSI SASA NDIYE MFALME WA MABAO ULAYA NZIMA KIHISTORIA

  BAO la penalti la Lionel Messi leo Barcelona ikiwatandika wenyeji Real Madrid 3-0 Uwanja wa Bernabeu katika mchezo wa La Liga linamfanya aafikishe jumla ya mabao 526 kwenye mashindano yote.
  Na sasa Messi anakuwa mfungaji bora wa muda wote katika Ligi tano kubwa Ulaya. 
  Kwa bao lake katika El Clasico ya leo, Messi moja kwa moja anakuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika klabu moja. 
  Anafikisha mabao 526 kwenye mashindano yote kwa Barcelona na maana yake anavunja rekodi ya gwiji wa Bayern Munich, Gerd Muller ya kufunga mabao mengi katika klabu mopja kwenye ligi tano kubwa Ulaya. 

  Lionel Messi sasa anakuwa mfungaji bora wa muda wote katika Ligi tano kubwa Ulaya PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Muller alifunga mabao 525 katika mechi 572 alizcheza Bayern Munich kati ya mwaka 1965 na 1979, wakati Messi amefunga mabao hayo katika jumla ya mechi 608 kwa timu hiyo ya Katalunya.
  Na Messi pia anaweza rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika El Clasico kuliko mchezaji yeyote katika historia ya mechi hizo jana akifikisha bao la 25 kwenye mechi 37 za mahasimu hao, akifuatiwa na gwiji wa Madrid, Alfredo di Stefano aliyefunga mabao 18 na Cristiano Ronaldo mabao 17. 
  Na ushindi wa leo unamaanisha Barcelona inaifunga Real Madrid kwa mara ya tatu mfululizo kwenye La Liga nyumbani kwake, Uwanja Bernabeu hii ikiwa ni mara ya kwanza kihistoria. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI SASA NDIYE MFALME WA MABAO ULAYA NZIMA KIHISTORIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top