• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 28, 2017

  MSUVAAAA….AFUNGA BAO PEKEE DIFAA WABEBA POINTI TATU LIGI YA MOROCCO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BAO pekee la winga wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happugod Msuva leo limeipa ushindi wa 1-0 Difaa Hassan El-Jadidi dhidi ya Hassania Agadir katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola.
  Msuva, mchezaji wa zamani wa Yanga alifunga bao hilo dakika ya 52 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan nchini Morocco.  
  Huo ni mwendelezo mzuri kwa Msuva tangu ahamie
  Morocco kufuatia kuwika katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kuwa Mfungaji Bora na Mchezaji Bora.
  Kikosi Difaa Hassan El Jadida kilikuwa; Yahia El Filali, M. Hahdhoudhi, Y. Aguerdoum, Bacary N’diaye, Anouar Jayid, Adil El Hasnaoui, Tarik Astati, Fabrice Ngah, Simon Msuva/Ayoub Nanah dk75, Bila El Magri/Mario Mandrault dk75 na Adnane El Quardy. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MSUVAAAA….AFUNGA BAO PEKEE DIFAA WABEBA POINTI TATU LIGI YA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top