• HABARI MPYA

  Jumanne, Desemba 26, 2017

  ZANZIBAR WATWAA UBINGWA WA KIMATAIFA SOKA LA UFUKWENI DAR

  Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM
  TIMU ya taifa ya Zanzibar ya soka la Ufukweni, imetwaa ubingwa wa Copa Dar es Salaam kwa kuifunga Malawi mabao 3-2 katika mechi ya fainali ya michuano hiyo iliyofanyika leo kwenye ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam.
  Zanzibar ilifanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo baada ya kuongoza kwenye msimamo wakiwa na pointi 6 wakifuatiwa na Malawi waliokuwa sawa nao kwa pointi lakini Zanzibar ikiwa juu kwa idadi kubwa ya mabao.
  Michuano hiyo ya Copa Dar es Salaam ilianza kutimua vumbi Desemba 25 mwaka huu kwenye fukwe za Coco, ikishirikisha jumla ya timu nne ambazo ni Tanzania Bara, Uganda, Malawi na Zanzibar.
  Wachezaji wa Zanzibar wakishangilia na Kombe lao la  ubingwa wa Copa Dar es Salaam baada ya kuifunga Malawi 3-2 katika mfainali leo kwenye ufukwe wa Coco, Dar es Salaam

  Zanzibar ilifanikiwa kutinga fainali katika Mashindano ya Copa Dar es salam baada ya asubuhi ya jana kuwachapa Malawi mabao 5-1, ambapo katika mchezo mwengine Uganda waliichapa Tanzania Bara kwa mabao 6-5.
  Michuano hiyo ya soka la ufukweni kwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati huku Malawi wakiwa ni waalikwa, ambapo mshindi ambaye ni Zanzibar amejinyakulia kombe pamoja na medali za dhahabu, mshindi wa pili (Malawi) wamepata medali za fedha na mshindi wa tatu ambaye ni Tanzania Bara wameondoka na medali za shaba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ZANZIBAR WATWAA UBINGWA WA KIMATAIFA SOKA LA UFUKWENI DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top