• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 24, 2017

  PAMBA SC WASAHAU KUREJEA LIGI KUU, WAAPA KUSALIA FDL

  Na Mwandishi Wetu, MWANZA
  BAADA ya hapo jana kupata ushindi katika mchezo wa kombe la Shirikisho la Azam kwa kuifunga Mufindi United kwa mikwaju ya Penalt mitatu kwa mmoja, Wanatipilindanda Pamba ya Mwanza wamejipanga kuhakikisha wanasalia katika ligi daraja la kwanza kwa nguvu zote ,hayo yamesemwa na kocha mkuu wa timu hiyo ambaye ni mchezaji wa zamani wa hapo pamba Venance Kazungu alipokua akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online
  ‘’Baada ya ushindi wa jana dhidi ya Mufindi nimewajenga vijana wangu katika hali ya kuapambana na katika hali ya ushindi,kwani nimesajili wachezaji sahihi na katika muda sahihi kama mambo yataenda kama nilivyopanga wakafata kile ambacho tunakifanya mazoezini kwa uvumilivuwao naamini na  nauhakika pamba  tutabaki ligi daraja la kwanza msimu huu na tupambane kurejea Premier Mwakani baada ya miaka kumi na saba’’
  Kikosi cha Pamba SC kikiwa Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza 
  Katika hatua nyingine Kazungu amewataka wana mwanza kuwa wamoja na kuonesha uzalendo kwa timu zao tatu zilizoko katika kundi moja la kundi c katika ligi daraja la kwanza Fdl huku akiomba chama cha soka mkoa wa mwanza Mzfa kilichoko chini ya Mwenyekiti Vedastus Lufano ambaye ni mjumbe wa kamati tendaji ya shirikisho la soka Tanzania tff akiwakilisha mikoa ya Mara na Mwanza kutoiangalia timu moja na badala yake itazame namna gani watazisaidia timu hizo katika ligi hiyo yenye ushindani mkubwa.
  Ikumbukwe Pamba yenye historia kubwa katika soka la Tanzania baada ya kutwaa ubingwa wa kombe la muungano na kupata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa, iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi kumi na mbili nyuma ya Alliance ya Mwanza,Dodoma fc ya Dodoma na Biashara ya Mara na wataanza duru ya mzunguguko wa kumi kwa kusafiri hadi mkoani Mara kuwakabili wenyeji Biashara zamani Police mara kwenye uwanja wa sabasaba wakati Alliance watasafiri hadi Dodoma kucheza Na Dodoma fc katika uwanja wa Mpwapwa ulioko nje kidogo ya mji wa Dodoma michezo yote itachezwa December  michezo mingine itakua inazikutanisha Toto Afrika dhidi ya Maafande wa Jkt Orjolo huku Transit Camp wakicheza na Ndugu zao Rhyno Rangers katika uwanja wa Ccm Kambarage mjini Shinyanga michezo yote itachezwa kati ya December thelathini na December thelathini na moja mwaka huu ambapo timu mbili zitapanda ligi kuu Tanzania bara baada ya mizunguko kumi na nne kukamilka
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PAMBA SC WASAHAU KUREJEA LIGI KUU, WAAPA KUSALIA FDL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top