• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 20, 2017

  BRAVO AIPELEKA MAN CITY NUSU FAINALI KOMBE LA CARABAO

  Kipa wa Manchester City, Claudio Bravo akishangilia baada ya kuokoa penalti za Jamie Vardy na Riyad Mahrez wa Leicester City na kuipa timu yake ushindi wa penalti 4-3 hivyo kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120. Waliofunga penalti za City ni İlkay Gundogan, Yaya Toure, Lukas Nmecha na Gaabriel Jesus wakati waliofunga za Leicester ni Christian Fuchs, Harry Maguire na Vicente Iborra.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa King Power, Bernardo Silva alianza kuifungia City dakika ya 26 kabla ya Vardy kuisawazishia Leicester kwa penalti dakika ya saba ya muda wa nyongeza baada ya kutimia kwa dakika 90 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BRAVO AIPELEKA MAN CITY NUSU FAINALI KOMBE LA CARABAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top