• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 23, 2017

  LIPULI YARIDHIA ASANTE KWASI KUHAMIA SIMBA

  Na Sada Hassan, DAR ES SALAAM
  HATIMAYE klabu ya Lipuli ya Iringa imeridhia beki wake wa kati, Mghana Asante Kwasi ajiunge na klabu ya Simba ya Dar es Salaam.
  Lipuli wameandikia barua TFF kuwathibitishia kwamba Simba SC wamefuata na kukamilisha taratibu za usajili wa Kwasi na sasa wamerishia uhamisho huo.
  Awali, Lipuli iligoma kumruhusu Kwasi kwenda Simba baada ya timu ya Dar es Salaam kutofuata taratibu za kumhamisha.
  Kwasi anakwenda kuchukua nafasi ya Mzimbabwe, beki wa kati, Method Mwanjali ambaye ameachwa kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe.
  Asante Kwasi (kulia) sasa anaungana na Mrundi Laudit Mavugo (kushoto) katika kikosi cha Simba

  Poppe, Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amesema kwamba katika dirisha hili dogo Simba imeacha na kusajili mchezaji mmoja mmoja tu wa kigeni ili kuimarisha kikosi chake.
  Kwasi anaondoka Lipuli baada ya miezi mitano ya kuchezea timu hiyo iliyopanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu tangu ajiunge nayo kutoka Mbao FC ya Mwanza.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIPULI YARIDHIA ASANTE KWASI KUHAMIA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top