• HABARI MPYA

        Thursday, December 28, 2017

        RATIBA MPYA MAPINDUZI, SIMBA KUFUNGUA DIMBA NA MWENGE, YANGA WAPEWA SINGIDA UNITED

        Na Salum Vuai, ZANZIBAR
        TIMU ya Singida United imeingizwa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi na itakuwa Kundi A pamoja na Yanga SC, Zimamoto, Mlandege, JKU na Taifa ya Jan’gombe.
        Kundi linabaki kuwa na timu za Simba, Azam FC, URA, Jamhuri na Mwenge baada ya kuondolewa kwa Taifa ya Jang’ombe iliyohamishiwa Kundi B ambako imeondolewa Shaba.
        Michuano ya Mapinduzi itaanza kesho kwa mechi kati ya Mlandege na JKU Saa 8:30 mchana, kabla ya Jamhuri kumenyana na Mwenge Saa 10:30 jioni na Zimamoto kupepetana na Taifa ya Jan’gombe Saa 2:15 usiku, zote zikichezwa Uwanja wa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

        Mabingwa watetezi, Azam FC wataanza mashindano Jumapili kwa kumenyana na Mwenge Saa 10:30 jioni kabla ya Jamhuri kumenyana na URA  Saa 2:15 usiku, wakati vigogo Simba na Simba wao wataanza mashindano Janauri 2, 2018. 
        Simba wataanza na Mwenge Saa 10:30 jioni wakati Saa 2:15 usiku Yanga watapepetana na Mlandege, mechi ambazo zitatanguliwa na mchezo kati ya Singida United na Zimamoto.
        Azam watarudi tena uwanjani Januari 3, 2018 kumenyana na Jamhuri SC Saa 10:30, baadaye URA Januari 5, 2018 Saa 10:30, kabla ya kukutana na Simba Januari 6 Saa 2:15 usiku kukamilisha mechi  zake za Kundi A.
        Simba watarudi uwanjani Januari 4 kumenyana na Jamhuri Saa 2:15 usiku, kabla ya kukutana na Azam Januari 6 na kuhitimisha mechi zake za Kundi A kwa kumenyana na URA Januari 8, 2018 Saa 10:30 jioni.
        Yanga wao watarudi uwanjani  Januari 4 Saa 10:30 jioni kumenyana na JKU, kabla ya kupepetana na Taifa ya Jan’gombe  Saa 2:15 usiku Januari 5, Zimamoto Saa 2:15 usiku Januari 7 na kukamilisha mechi zake za Kundi B Januari 8 kwa kumenyana na Singida United.
        Mechi za makundi zinatarajiwa kukamilishwa Januari 8, wakati Januari 9 itakuwa mapumziko na Nusu Fainali zitafuatia Januari 10, kabla ya kilele mashindano kwa mchezo mtamu wa fainali Januari 13, ambao utahudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi visiwani humo, Dk. Ali Mohammed Shein.


        MAKUNDI:
        KUNDI A: URA; Jamhuri; Mwenge; Azam; Simba.
        KUNDI B: Zimamoto; Mlandege; Yanga; JKU; Taifa ya Jan’gombe; Singida United.
        RATIBA KAMILI:
        Desemba 29, 2017
        Mlandege vs JKU  (Saa 8:30 mchana)
        Jamhuri vs  Mwenge (Saa 10:30 jioni)
        Zimamoto vs Taifa ya Jan’gombe (Saa 2:15 usiku)
        Desemba 30, 2017
        Zimamoto  vs JKU (Saa 10:30 jioni)
        Taifa ya Jan’gombe vs Mlandege (Saa 2:15 usiku)
        Desemba 31, 2017
        Azam    vs   Mwenge (Saa 10:30 jioni)
        Jamhuri vs URA (Saa 2:15 usiku)
        Januari 1, 2018
        Mlandege  vs  Zimamoto (Saa 10:30 jioni)
        JKU vs   Taifa ya Jan’gombe (Saa 2:15 usiku)
        Januari 2, 2018
        Singida United  vs Zimamoto (Saa 8:30 mchana)
        Simba  SC  vs Mwenge (Saa 10:30 jioni)
        Yanga   vs   Mlandege  (Saa 2:15 usiku)
        Januari 3, 2018
        URA vs   Mwenge (Saa 8:30 mchana)
        Azam  FC vs   Jamhuri (Saa 10:30 jioni)
        Taifa Jan’gombe vs Singida United (Saa 2:15 usiku)
        Januari 4, 2018
        JKU vs Yanga (Saa 10:30 jioni)
        Simba  vs   Jamhuri (Saa 10:30 jioni)
        Januari 5, 2018
        Mlandege  vs  Singida United (Saa 8:30 mchana)
        URA    vs   Azam (Saa 10:30 jioni)
        Yanga   vs  Taifa Jan’gombe (Saa 2:15 usiku)
        Januari 6, 2018
        JKU   vs  Singida United (Saa 10:30 jioni)
        Simba    vs   Azam FC (Saa 2:15 usiku)
        Januari 7, 2018
        Zimamoto FC vs  Yanga SC (Saa 10:30 jioni)
        Januari 8, 2018
        Simba SC vs URA (Saa 10:30 jioni)
        Yanga SC vs  Singida United  (Saa 10:30 jioni)
        Januari 9, 2018
        MAPUMZIKO
        Januari 10, 2018
        NUSU FAINALI
        Mshindi Kundi A Vs Mshindi wa Pili Kundi B (Saa 10:30 jioni)
        Mshindi Kundi B Vs Mshindi wa Pili Kundi A (Saa 2:15 usiku)
        Januari 13, 2018
        FAINALI 
        (Saa 2:00 usiku)
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: RATIBA MPYA MAPINDUZI, SIMBA KUFUNGUA DIMBA NA MWENGE, YANGA WAPEWA SINGIDA UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry