• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 21, 2017

  KAGERA SUGAR YAICHAPA 7-0 MAKAMBAKO KOMBE LA AZAM SPORTS, ALLIANCE NJE MAPEMAAA

  Na Waandishi Wetu, KAGERA NA TABORA
  TIMU ya soka ya Kagera Sugar imekwenda hatua ya 32 Bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 7-0 dhidi ya Makambako Uwanja wa Kaitaba, Bukoba joni ya leo.
  Mshambuliaji mkongwe, Themi Felix Buhaja leo alikuwa ana siku nzuri baada ya kufunga mabao matatu peke yake, la kwanza kwa penalti dakika ya 14 na mengine dakika za 39 na 48.
  Mabao mengine ya Kagera Sugar ya kocha Mecky Mexime yamefungwa na Venance Ludovick dakika ya 19, Peter Mwalyanzi mawili dakika za 63 na 90 na Mwahita Saleh Gereza dakika ya 84.
  Themi Felix (kulia) leo amefunga mabao matatu katika ushindi wa 7-0 wa Kagera Sugar PICHA YA MAKTABA

  Mchezo mwingine, Alliance FC ya Mwanza imetolewa baada ya kufungwa 1-0 na wenyeji, Rhino Rangers leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.
  Bao lililoitupa nje Alliance katika hatua ya 64 Bora ya mashindano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilifungwa na Mbwana Juma dakika ya 25 akitumia makosa ya mabeki wa timu hiyo kuchanganyana.
  Kocha Msaidizi wa Alliance, Kessy Mziray alisema baada ya mchezo huo kwamba timu yake ilikposa bahati katika mchezo wa leo, kwani ilicheza vizuri na kutengeneza nafasi lakini ikashindwa kuzitumia.
  Kwa matokeo hayo, Rhino inatinga hatua ya 32 bora ikiungana na timu za Njombe Mji iliyoifunga Mji Mkuu ya Dodoma 2-0, Majimaji Rangers walioifunga Mbeya Kwanza 1-0, Toto Africans, KMC, Nadanda FC, Polisi Tanzania walioifunga Mshikamano 2-1 na JKT Orjolo ya Arusha iliyowafunga wenyeji, Ambassador ya Kahama mkoani Shinyanga kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 1-1.
  Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi za Green Warriors na Simba; Polisi Dar na Mgambo JKT ya Tanga; Kariakoo ya Lindi na Transit Camp ya Dar ila kwa sasa imeweka maskani Shinyanga; Biashara ya Mara itacheza na Mawenzi Market ya Morogoro; Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani itacheza na Madini FC ya jijini Arusha huku Mufindi United na Pamba ya Mwanza ilihali Singida United itacheza na Bodaboda FC.
  Mchezo kati ya Simba na Green Warriors utaochezwa Desemba 22, utakuwa ni maalumu kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa michuano hiyo msimu. Sababu Simba ndiye bingwa mtetezi.
  Siku ya Desemba 23, mwaka huu Azam FC itacheza na Area C; African Lyon ya Dar es Salaam na Kiluvya United ya Pwani; Makanyagio itapambana na Mbao; Mwadui na Pepsi; Majimaji na New Generation wakati Mbeya City itacheza na Ihefu.
  Desemba 24, 2017 Yanga SC itacheza na Reha FC; Burkina ya Morogoro na Lipuli ya Iringa;  Coastal Union ya Tanga na Dodoma Fc ya Dodoma; Shupavu na Real Mojamoja wakati Villa Squad itacheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAICHAPA 7-0 MAKAMBAKO KOMBE LA AZAM SPORTS, ALLIANCE NJE MAPEMAAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top