• HABARI MPYA

  Tuesday, October 03, 2017

  SIMBA KUMENYANA NA DODOMA FC KESHO JAMHURI

  Na Rehema Lucas, DODOMA
  SIMBA SC imewasili mjini Dodoma leo tayari kwa mchezo wa kirafiki na wenyeji, Dodoma FC kesho Uwanja wa Jamhuri mjini humo.
  Mkuu wa Idara ya Habari ya Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Sunday Manara amesema leo mjini hapa kwamba wanauoa uzito mchezo huo kwa sababu ni sehemu ya maandalizi yao ya mechi ijayo ya Ligi Kuu.
  Manara amesema kwamba ni mchezo ambao wachezaji ambao hawana nafasi kikosi cha kwanza watapata fursa ya kucheza, kufuatia wenye namba zao kwenda kujiunga na timu ya taifa, Taifa Stars.
  Msemaji wa Simba SC, Hajji Manara (katikati), akizungumzia maandalizi ya mchezo dhidi ya Dodoma FC kesho Uwanja wa Jamhuri 

  Manara amesema anaamini wachezaji watakaopewa nafasi wataitumia vizuri fursa hiyo kwa kuonyesha uwezo ili kumshawishi kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog awaamini kwa michezo ijayo.
  Kwa upande wake, Afisa Habari wa Dodoma FC, Recardo Sylvester amesema mchezo huo ni fursa nzuri kwao kujipima timu kongwe nchini, yenye wachezaji bora kutoka nchi tofauti.
  Sylvester amesema kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ anataka kuutumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mechi zao za Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
  Kwa Simba mchezo huu, ni mwendelezo wa utaratibu wake wa kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Daraja la Kwanza katikati ya mechi zake za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Baada ya kutoka sare ya 2-2 na Mbao FC mjini Mwanza katika mechi ya Ligi Kuu, Simba ilkwenda Tabora kucheza mechi ya kirafiki na Rhino Rangers Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjii Tabora na kutoa sare ya 0-0.
  Na sasa ikitoka kushinda 2-1 dhidi ya Stand United Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Simba itacheza na Dodoma FC mchezoi wa kirafiki kesho kuelekea mechi yake ijayo ya Ligi Kuu na Mtibwa Sugar Oktoba 15, mwaka huuu Uwanja wa Uhuru.        
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA KUMENYANA NA DODOMA FC KESHO JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top