• HABARI MPYA

  Wednesday, October 04, 2017

  MENEJA WA MPINZANI WA EUBANK ATAKA KUZIPIGA KAVU KAVU MKUTANONI

  MENEJA wa Avni Yildirim, Ahmet Oner amemuita mpinzani wa bondia wake Chris Eubank Jnr 'kiburi' kabla ya kutaka kupigana na mmoja wa wafuasia wa bondia huyo wa Uingereza katika mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu pambano lao ubingwa wa dunia.
  Eubank na Yildirim watapambana mjini Stuttgart, Ujerumani Jumamosi katika pambano la pili la Robo Fainali la uzito wa Super Middle kwenye michuano ya mabondia wanane.
  Mabondia hao walikutana uso kwa uso Jumatano kwenye mkutano na Waandishi wa Habari siku moja baada ya Eubank Jnr kushindwa kutokea kwa matembezi ya kulitangaza pambano hilo nchini Ujerumani – na baba yake, Chris Snr akasema alisitisha mpango huo kwa kuhofia usalama wa mwanawe kutokana na vurugu za Waturuki.

  Chris Eubank Jr (kulia) na Anni Yildirim (kushoto) wakiwa wametulia kwenye mkutano na Waandishi wa Habari, huku Ahmet Oner (kushoto kabisa) akitaka kupigana PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Baada ya mabondia wote kuzungumza kuelekea pambano lao hilo la Jumamosi, Oner, meneja na kocha wa bondia wa Uturuki, akaanza kuwasemea ovyo Eubank na baba yake kabla ya kusimama na kutaka kupigana na mmoja wa wana msafara wa wapinzani wao.
  "Nitakutupa nje,"alifoka, wakati wote Eubank na Yildirim wakiwa wametulia kama hawaoni kinachoendelea huku kocha huyo akiendelea kuropoka maneno machafu.
  Meneja huyo akarejeshwa katika meza ya mkutano, lakini akainuka tena na kuvua jaketi lake akitaka kupigana na mtu yule yule wa timu ya Eubank huku akisema: "Usinichekee mimi!' 
  Baadaye meneja wa Yildrim alirejea chumbani huku akitoa maneno machafu. Mabondia hao nao walitambiana kuelekea pambano lao, kila mmoja akitamba kumchakaza mwenzake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MENEJA WA MPINZANI WA EUBANK ATAKA KUZIPIGA KAVU KAVU MKUTANONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top