• HABARI MPYA

  Tuesday, October 03, 2017

  BABBEL: RIBERY ANAJIONA KAMA MESSI NA RONALDO WAKATI 'AMEISHA'

  WACHEZAJI wengi wa Bayern Munich wanajiona kama wa kiwango cha dunia licha ya kuboronga kwa klabu hiyo siku za karubini.
  Hayo yamesemwa na beki wa zamani wa Bayern Munich, Markus Babbel, ambaye amemtaja Franck Ribery kama sababu ya kufukuzwa kwa kocha Carlo Ancelotti baada ya mwaka mmoja tu wa kuwa kazini. 
  Babbel, ambaye pia alichezea Liverpool, amesema wengi kati ya wachezaji wa Bayern wanaishi kwa mafanikio ya zamani, akimtaja Ribery kama galasa zaidi.
  "Franck Ribery hajafunga hata bao moja kwenye Ligi ya Mabingwa kwa miaka miwili iliyopita. Bado anajiona yuko kwenye kiwango sawa na akina Cristiano Ronaldo au Lionel Messi, lakini ukweli ni tofauti. Ukweli ni kwamba hayuko huko,".

  Franck Ribery ametajwa na Markus Babbel kama mmoja wa wachezaji wanasababisha matokeo mabaya Bayern Munich PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


  "Ni jambo la kusikitisha kwamba mzigo wote anatupigwa Carlo Ancelotti. Ribery ana heshima kubwa kwa klabu na amekuwa mchezaji mzuri, lakini nafasi anayoihodhi kwa sasa, kwa mtazamo wangu naona hawezi kuimudu," amesema Babbel. 
  Bayern ilishinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya mwisho mwaka 2013, na Ribery, mwenye umri wa miaka 34 sasa, akicheza fainali Uwanja wa Wembley.
  Hata hivyo, kipigo cha mabao 3-0 katika mchezo wa hatua ya makundi kutoka kwa PSG kinaifanya bodi ya Bayern imfukuze Ancelotti licha ya kushinda taji la Bundesliga katika msimu wake pekee kamili kwenye klabu.
  Ribery sasa anatarajiwa kukosa sehemu kubwa ya msimu iliyobaki, baada ya kutonesha maumivu ya goti katika mchezo wa Bayern Munich na Hertha Berlin uliomalizika kwa sare ya 2-2.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BABBEL: RIBERY ANAJIONA KAMA MESSI NA RONALDO WAKATI 'AMEISHA' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top