• HABARI MPYA

  Thursday, September 14, 2017

  TIMU YA ABDI BANDA YAMFUKUZISHA KOCHA AFRIKA KUSINI

   KLABU ya Chippa United imethibitisha kumfukuza kocha wake, Dan Malesela kufuatia kipigo cha mabao 3-1 nyumbani kutoka kwa timu ya Baroka FC, anayochezea beki Mtanzania, Abdi Hassan Banda juzi Uwanja wa Nelson Mandela Bay katika mchezo wa Ligi Kuu ya ABSA ya Afrika Kusini.
  Hicho kilikuwa kipigo cha pili kwa Chippa katika mechi tatu za mwanzo za Ligi Kuu baada ya kufungwa pia na Orlando Pirates kwenye mchezo wa ufunguzi. Matokeo yao mengine ni ushindi wa nyumbani dhidi ya AmaZulu kabla ya kwenda kwenye mapumziko ya mechi za kimataifa.
  Chippa United imethibitisha kumfukuza kocha Dan Malesela kufuatia kipigo cha mabao 3-1 nyumbani kutoka kwa Baroka FC 

  Baada ya hatua hiyo, Malesela amesema ameshangazwa na hatua ya klabu kuchukua uamuzi wa kumvinjia mkataba. Amewaambia Waandishi wa Habari kwamba; “Ndiyo, nimefukuzwa. Haijanishitua sana kwa sababu nilitarajia hili,” alisema.
  “Ukiwa unafanya kazi katika hii klabu unatarajia chochote. Sifikiri kama nitarudi tena Port Elizabeth daima, sifikirii kama nitafanya hivyo,” alisema.
  Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 alitofautiana na uongozi wa klabu hiyo alipokuwa kazini na Chilli Boys. Msimu uliopita alipewa likizo, kabla ya kurejeshwa na kuisaidia Chippa kunusurika kushuka daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIMU YA ABDI BANDA YAMFUKUZISHA KOCHA AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top