• HABARI MPYA

  Thursday, September 14, 2017

  MAYWEATHER ANA WANAWAKE SABA, GARI 25 NA "PESA CHAFU"

  BONDIA Floyd Mayweather amesema kwamba anamiliki wapenzi saba kwa wakati mmoja na pia ana akaunti nyingi za benki ambayo kila moja ina kati ya dola za Kimarekani Milioni 200 hadi 300.
  Akizungumza na Diego kutoka chaneli ya YouTube ya Awkward Puppets, Mayweather amesema kwamba ana marafiki wa kike saba na gari 25 mjini Las Vegas pekee, zikiwemo Bugatti nyekundu na Ferrari ya njano.
  Mayweather pia amesistiza kwamba pambano dhidi ya Conor McGregor Agosti mwaka huu ndiyo lilikuwa pambano lake la mwisho kupanda ulingoni kupigana.
  Floyd Mayweather amesema katika akaunti moja ya benki anamiliki kati ya dola Milioni 200 na Milioni 300 PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  “Pambano la mwisho nililopigana, hilo lilikuwa pambano la fedha,”amesema Mayweather. “Kwa kweli, kwa sababu pambano lingine wakijaribu kunishawishi, nitapigana katika ulimwengu mwingine,” amesema.
  Mayweather alikuwa anazungumza na Diego kwenye klabu ya starehe iitwayo Girl Collection mjini Las Vegas na alipoulizwa kama ana mpenzi alisema yeye si mwanaume wa kujifunga kwa mwanamke mmoja.
  “Nina wanawake wangapi? Inawezekana kama saba hivi,” amesema Mayweather. “Tunakwenda nje kula, baadhi tunasafiri pamoja. Kuwa na mmoja ni sawa kutokuwa naye kabisa,”. 
  Diego pia aliuliza kiasi cha fedha alichonacho bondia huyo katika utajiri wake na Mayweather akamuambia ana akaunti kadhaa za benki kabla ya kusema ana kiasi gani fedha. 
  “Dola Milioni 200, dola Milioni 300, ndio. Katika akaunti tofauti,”amesema.
  Mayweather alilipwa kiasi cha dola za Kimarekani Milioni 100 kwa pambano lake moja tu dhidi ya McGregor mwezi Agosti. Alimpiga mbabe huyo wa Ireland kwa Knockout (KO) raundi ya 10 kupata ushindi wake wa 50 mfululizo katika historia ya kutopoteza pambano hata moja hadi anastaafu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYWEATHER ANA WANAWAKE SABA, GARI 25 NA "PESA CHAFU" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top