• HABARI MPYA

  Friday, September 08, 2017

  RAYON KUFUNGUA DIMBA NA AS KIGALI LIGI KUU YA AZAM RWANDA

  Na Canisius Kagabo, KIGALI
  MABINGWA wa Ligi Kuu ya Azam Rwanda, Rayon Sports wataanza kutetea taji lao katika msimu mpya kwa kumenyana na AS Kigali Septemba 29, Uwanja wa Kigali, Nyamirambo.
  Hiyo ni katika Ratiba ya Ligi Kuu ya Azam Rwanda maarufu kama ‘Azam Rwanda Premier League’, msimu wa 2017/2018 iliyotolewa jana Shirikisho la Soka nchini Rwanda (FERWAFA).
  Kikao cha Kamati ya Utendaji ya FERWAFA kilichofanyika jana kiliamua kwamba ligi inapaswa kuanza mwishoni mwa mwezi wa Septemba na kuwakumbusha viongozi wa klabu kutafuta vitambulisho (license) vya wachezaji wake mapema.
  “Nataka kuwaambia kwamba leo kamati ya Utendaji ya FERWAFA tumefanya kikao kirefu, tumethibitisha kwamba ligi itaanza tarehe 29 mwezi Septemba mwaka 2017. Tunawakumbusha viongozi wa klabu kutafuta vitambulisho vya wachezaji wao mapema,” amesema Makamu wa Rais wa FERWAFA, Kayiranga Vedaste. 
  Si kawaida kwa Ligi Kuu ya Azam Rwanda kuanza mapema, lakini msimu huu FERWAFA imeonyesha mabadiliko mapema, kuashiria msimu mpya utakuwa mzuri.

  RATIBA YA MECHI ZA UFUNGUZI LIGI KUU YA AZAM RWANDA
  Septemba 29, 2017
  Rayon Sports vs AS Kigali
  Septemba 30, 2017
  APR FC vs Sunrise FC
  Etincelles FC vs Police FC
  Gicumbi FC vs Espoir FC
  Kirehe FC vs Mukura VS
  Oktoba 1, 2017
  Bugesera FC vs Amagaju FC
  Miroplast FC vs Marines FC
  Kiyovu Sports vs Musanze FC
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAYON KUFUNGUA DIMBA NA AS KIGALI LIGI KUU YA AZAM RWANDA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top