• HABARI MPYA

  Wednesday, September 06, 2017

  NDUDA KWENDA INDIA WIKIENDI HII, KIINGILIO SIMBA NA AZAM...

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KIPA wa pili wa Simba, Said Mohammed Kasarama ‘Nduda’ anatarajiwa kusafirishwa mwishoni mwa wiki kupelekwa India kwa matibabu la mguu wake wa kushoto.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Hajji Sunday Manara ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba Ndunda maandalizi ya safari yake yamekwishakamilika na wikiendi hii Nduda atasafirishwa.
  “Kila kitu kimekaa vizuri kwa maana ya mazungumzo ya hospitali atakayokwenda kutibiwa yamekwishafanyika na siku maalum ya kufika amekwishapangiwa na ni matarajio yetu wikiendi kijana ataenda India kufanyiwa matibabu hayo,”amesema.  
  Said Mohammed anatarajiwa kupelekwa India kwa matibabu ya goti lake la mguu wa kushoto


  Kipa huyo bora wa michuano ya COSAFA mwaka huu nchini Afrika Kusini, aliyesajiliwa Julai kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, aliumia katika kambi ya Zanzibar kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu, Yanga SC Agosti 23, mwaka huu.
  Simba ilishinda kwa penalti 5-4 baada ya sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam langoni akiwa kipa namba moja, Aishi Salum Manula.
  Aidh, Hajji mtoto wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Sunday Manara ‘Kompyuta’ amesema kwamba wachezaji wengine waliokuwa majeruhi kiungo Haruna Niyonzima na mshambuliaji John Raphael Bocco wamekwishaanza mazoezi kujiandaa na mechi dhidi ya Azam FC Jumamosi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Wakati huo huo: Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetaja viingilio vya mchezo kati ya Azam na Simba Jumamosi, ambavyo ni Sh. 10,000 kwa V. I. P na Sh 7,000 kwa mzunguko.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NDUDA KWENDA INDIA WIKIENDI HII, KIINGILIO SIMBA NA AZAM... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top