• HABARI MPYA

  Wednesday, September 13, 2017

  MBEYA CITY YAACHANA RASMI NA PHIRI, KIJUSO APEWA MIKOBA

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  KLABU ya Mbeya City FC leo imesitisha mkataba na aliyekuwa kocha wake Mkuu, Mmalawi Kinnah  Phiri.
  Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha kilichofanyika leo mjini Mbeya, kufuatia malalamiko ya kocha huyo kutolipwa mishaharakwa miezi mitano kiasi cha kususa. 
  Kikao cha leo kilikuwa ni mwendelezo wa vikao kadhaa baina ya pande hizo mbili tangu Julai mwaka huu na baada ya majadiliano marefu, Mbeya City na Phiri wamekubaliana kutoendelea kufanya kazi pamoja.
  "Sababu kubwa ni matokeo mabaya ya timu ya msimu uliopita 2016/2017 ambayo yameipunguzia klabu uwezo mkubwa wa kuhimili mahitaji yake ya msingi baada ya wadhamini waliotarajia kuingia kushindikana na wadhamini waliopo kupunguza kiwango cha udhamini wao kutokana na matokeo hayo yasiyoridhisha,"imesema taarifa ya Mbeya City.
  Kocha Mmalawi, Kinnah  Phiri leo ametupiwa virago rasmi Mbeya City

  Wakati uongozi ukiendelea kutafuta kocha mpya, kwa sasa Mbeya Citu ipo chinio ya mchezaji wake wa zamani na aliyekuwa Kocha Msaidizi tangu wakati wa Juma Mwambusi, Mohammed Kijuso."Klabu inapenda kumshukuru Kocha Phiri kwa mchango wake muhimu katika timu yetu, itaendelea kuuthamini na kuukumbuka na inaamini Kocha Phiri ataendelea kuwa msaada katika maendeleo ya timu yetu kwani amekuwa sehemu ya familia yetu,"imesema taarifa ya MCC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAACHANA RASMI NA PHIRI, KIJUSO APEWA MIKOBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top