• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 21, 2015

  WANGA: TUMEKUJA KUWARINGISHIA NA KURUDI NALO NYUMBANI KOMBE LETU

  MSHAMBULIAJI tegemeo wa Kenya, Alan Wanga amesema kwamba wanataka kutetea Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge nchini Kenya.
  Wanga anayechezea Azam FC ya Tanzania amesema kwamba Kenya ina kikosi kizuri chenye damu mchanganyiko, kikihusisha pia wachezaji wenye uzoefu na chipukizi, hivyo wanaamini wanaweza kubeba taji.
  Amesema anaamini michuano itakuwa migumu, lakini wamejipanga vizuri kuhakikisha wanarejea na Kombe lao nyumbani.
  Allan Wanga amesema Kenya watarudi na Kombe lao Nairobi

  “Mpira wa huku kwetu hautofautiani sana, tunazidiana vitu vidogo vidogo tu, maana yake ushindani utakuwa mkubwa, lakini Harambee Stars tuko vizuri na tunataka kurudi na Kombe letu Nairobi,” amesema Wanga aliyekuwa nyota wa kikosi kilichotwaa Kombe hilo mwaka juzi nyumbani.
  Challenge inatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo nchini Ethiopia wenyeji wakifungua dimba na Rwanda mjini Addis Ababa.
  Mchezo huo wa Kundi A utatanguliwa na mechi nyingine ya Kundi B, kati ya Burundi na Zanzibar.
  Tanzania Bara watatupa kete yao ya kwanza kesho, watakapomenyana na Somalia katika mchezo wa Kundi A, wakati mabingwa watetezi, Kenya watasuguana na mabingwa wa kihistoria, Uganda baadaye. 
  Mechi za mzunguko wa kwanza wa makundi zitakamilishwa keshokutwa, Sudan Kusini wakimenyana na Djbouti kabla ya Sudan na Malawi kufuatia baadaye.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WANGA: TUMEKUJA KUWARINGISHIA NA KURUDI NALO NYUMBANI KOMBE LETU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top