• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 21, 2015

  KAVUMBANGU ‘AWAUA’ ZANZIBAR, BURUNDI YAANZA VYEMA ADDIS 2015

  BAO pekee la Didier Kavumbangu limeipa Burundi mwanzo mzuri katika michuano ya Kombe la Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kuilaza Zanzibar 1-0 jioni hii Uwanja wa Taifa wa Addis Ababa, Ethiopia.
  Katika mchezo huo wa kundi B uliokuwa mkali na wa kusisimua, Kavumbangu anayechezea Azam FC ya Dar es Salaam alifunga bao hilo pekee dakika ya 22.
  Mchezo wa pili na wa ufunguzi rasmi wa michuano hayo mwaka huu, unafuatia sasa kati ya wenyeji Ethiopia dhidi ya Rwanda, ambao utakuwa wa Kundi A.
  Didier Kavumbangu amewalaza Zanzibar ufunguzi Kombe la Challenge

  Kikosi cha Zanzibar kilikuwa: Mwadini Ali, Nassoro Massoud ‘Chollo’, Mwinyi Hajji, Haidari Issa, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mudathir Yahya, Suleiman Kassim ‘Selembe’/Mateo Anthony, Mcha Khamisi, Awadh Juma Awadh, Ame Ali na Abrahamani Mohammed
  Burundi: MacArthur Arakaza, Karim Nizigiyimana, Fataki Kiza, David Nshimirimana, Issa Hakizimana, Yusuf Ndikumana, Fuwadi Ndayisenga, Cedric Amissi, Shashiri Nahimana, Didier Kavumbangu na Laudit Mavugo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAVUMBANGU ‘AWAUA’ ZANZIBAR, BURUNDI YAANZA VYEMA ADDIS 2015 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top