• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 22, 2015

  STARS WAFANYA MAUWAJI CHALLENGE, WAIPA SOMALIA ADHABU KAMA WALIYOPEWA REAL MADRID NA BARCELONA JANA

  Na Mwandishi Wetu, ADDIS ABABA
  TANZANIA Bara, Kilimanjaro Stars imeanza vyema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kuifunga Somalia mabao 4-0 jioni ya leo Uwanja wa Taifa wa Addis Ababa, Ethiopia.
  Matokeo hayo, yanaifanya Kili Stars inayofundishwa na mkongwe, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ ianzie kileleni mwa Kundi A ikiwashusha Rwanda walioifunga Ethiopia 1-0 jana. 
  Nahodha John Raphael Bocco ‘Adebayor’ amefunga mabao mawili katika ushindi huo, moja kwa penalti dakika ya 12 baada ya beki wa kulia, Shomary Kapombe kuangushwa na lingine dakika ya 54. 
  Elias Maguri (kulia) amefunga mabao mawili leo Kili Stars ikiua 4-0 Challenge

  Mshambuliaji pacha wake leo, Elias Maguri naye akafunga mabao mawili dakika ya 17 na 66 kukamilisha kipigo kama ambacho Barcelona iliipa Real Madrid jana katika La Liga Uwanja wa Bernabeu.
  Kipa Aishi Manula aliyeanza leo alifanya kazi nzuri ya kuokoa michomo mingi ya hatari langoni mwake na kujizolea sifa kemkem.
  Kikosi cha Tanzania Bara leo kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Kevin Yondan, Salum Mbonde, Himid Mao, Simon Msuva/Malimi Busungu dk71, Said Ndemla, Johm Bocco, Elias Maguri na Deus Kaseke. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STARS WAFANYA MAUWAJI CHALLENGE, WAIPA SOMALIA ADHABU KAMA WALIYOPEWA REAL MADRID NA BARCELONA JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top