• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 21, 2015

  MAN UNITED YAPANDA KILELENI LIGI KUU ENGLAND, YAICHAPA WATFORD 2-1

  MANCHESTER United imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Watford Uwanja wa Vicarage Road. 
  United inafikisha pointi 27 baada ya mechi 13 ikiwazidi kwa pointi moja mahasimu, Manchester City na Arsenal ambao wana mechi moja mkononi. City wataikaribisha Liverpool baadaye, wakati Arsenal watakuwa ugenini kwa West Bromwich Albion.
  Nyota wa Manchester United, Bastian Schweinsteiger (kulia) akishangilia baada ya krosi yake kuipa timu yake bao la ushindi, kufuatia mshambuliaji wa Watford, Troy Deeney kujifunga dakika ya 90 PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Katika mchezo wa leo, Memphis Depay alianza kuifungia Manchester United dakika ya 11, akimalizia krosi ya Ander Herrera, ambaye alitoka kipindi cha kwanza baada ya kuumia nyama na nafasi yake kuchukuliwa na Marcos Rojo.  
  Watford ilisawazisha bao hilo kwa penalti dakika ya 87 kupitia kwa Troy Deeney, baada ya Rojo kumchezea rafu Odion Ighalo
  Lakini mshambuliaji huyo wa The Hornets akajifunga dakika ya 90 katika harakatiza kuokoa krosi ya Bastian Schweinsteiger na kuipa United ambayo iliwakosa Wayne Rooney na Anthony Martial leo ushindi wa ugenini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAPANDA KILELENI LIGI KUU ENGLAND, YAICHAPA WATFORD 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top