• HABARI MPYA

  Jumanne, Novemba 24, 2015

  UGANDA YAIPIGA 4-0 ZENJI, WACHEZAJI WA AZAM WALIMWA KADI NYEKUNDU

  UGANDA imezinduka katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Zanzibar jioni ya leo mjini Addis Ababa, Ethiopia.
  Huo unakuwa mchezo wa pili mfululizo kwa Zanzibar Heroes kufungwa, baada ya awali kugungwa 1-0 na Burundi na sasa inajiweka katika mazingira magumu kwenda Robo Fainali.
  Mabao ya Uganda katika mchezo huo wa Kundi B yamefungwa na Farouk Miya dakika ya 10 na 18, Erisa Ssekisambu dakika ya 48 na Ceasar Okhuti dakika ya 79.

  Zanzibar ilipoteza wachezaji wawili kwa kadi nyekundu katika mchezo huo, kwanza kipa wake Mwadini Ally dakika ya 13 na baadaye kiungo Mudathir Yahya dakika ya 74, wote wa Azam FC ya Dar es Salaam. Zanzibar itamaliza na Kenya wakati Uganda itamaliza na Burundi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UGANDA YAIPIGA 4-0 ZENJI, WACHEZAJI WA AZAM WALIMWA KADI NYEKUNDU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top