• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 26, 2015

  HATIMAYE SIKU IMEWADIA, MASHAUZI CLASSIC KUZINDUA ALBAM MPYA LEO USIKU MANGO GARDEN

  LEO usiku ndani ya ukumbi wa Mango Garden Kinondoni kutakuwa na tukio kubwa la kiburudani ambapo Mashauzi Classic Modern Taarab, watazindua albam yao mpya ya “Sura Surambi”. 
  Uzinduzi wa albam hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa, utasindikizwa na kundi kongwe la taarab - East African Melody.
  Mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Mashauzi ameiambia JAMBO LEO kuwa albam ya “Sura Surambi” inaundwa na nyimbo sita kali.
  Isha amezitaja nyimbo hizo kuwa ni pamoja na “Sura Surambi” aliouimba yeye, “Kupendwa Bahati Yangu” uimbaji wake Abdumalick Shaaban, na “Mjinga Mpe Cheo” wa Zubeida Malick.
  Nyimbo nyingine alizozitaja Isha ni “Pendo la Ukakasi” wa Saida Ramadhan, “Ubaya Haulipizwi” ulioimbwa na Asia Mzinga na “Mapenzi Yamenivuruga” mwimbaji akiwa ni Naima Mohamed. Nyimbo zote hizo sita zimetungwa na Isha Mashauzi.
  Mbali na East African Melody, mkali wa tungo za mahaba Cassim Mganga naye pia atasindikiza uzinduzi huo wa albam ya “Sura Surambi”.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HATIMAYE SIKU IMEWADIA, MASHAUZI CLASSIC KUZINDUA ALBAM MPYA LEO USIKU MANGO GARDEN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top