• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 20, 2015

  MAGURI: SIMBA HATA WANIPE MLIMA KILIMANJARO SIRUDI NG’O

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI Elias Maguri amesema kwamba anaweza kujiunga na timu yoyote, lakini si Simba SC tena.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE jana Dar es Salaam, Maguri amesema kwamba hataki kabisa kurejea Simba SC na zaidi anafikiria kwenda kucheza nje.
  “Mimi kwa sasa nina mtu ambaye ananisimamia, huyo ndiye anazungumzia mambo yangu. Ila tu niseme wazi, naweza kujiunga na timu yoyote, lakini siyo Simba, hata wanipe mlima wa Kilimanjaro, sitaki kabisa,”amesema.
  Elias Maguri amesema Simba SC hata wampe mlima Kilimanjaro hatarejea Msimbazi

  Maguri ndiye anaongoza kwa mabao katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara hivi akiwa amefunga mara tisa katika mechi 10 alizocheza Stand United ya Shinyanga.
  Mshambuliaji huyo aliachwa Simba SC msimu huu baada ya kocha Muingereza, Dylan Kerr kusema anapoteza nafasi nyingi za kufunga.
  Na aliondoka Simba SC baada ya kuichezea mechi 43 na kuifungia mabao 12 kwa msimu mmoja, tena zaidi akitokea benchi.
  Maguri aliifunga timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars bao la kwanza katika sare ya 2-2 na Algeria Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Taifa Stars ilitolewa na Algeria katika mchujo wa kuwania tiketi ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi, baada ya kufungwa 7-0 katika mchezo wa marudiano Jumanne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAGURI: SIMBA HATA WANIPE MLIMA KILIMANJARO SIRUDI NG’O Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top