• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 16, 2015

  'KING KIBADENI' ATAJA KIKOSI CHA UBINGWA CHALLNGE 2016 ADDIS

  Na Mwandishi Wetu, ALGIERS
  KOCHA mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Alhaj Abdallah Athumani Seif 'King Kibadeni' ametangaza kikosi cha wachezaji 21 kujiandaa na michuano ya Kombe la Chalenji itakayoanza kutimua vumbi Jumamosi Novemba 21, nchini Ethiopia.
  Kibadeni anayesaidiwa na kocha msaidizi Juma Mgunda, amesema wachezaji aliowaita wapo katika hali nzuri na wamekua wakifanya mazoezi na kikosi cha Taifa Stars ambapo wao kama benchi la ufundi wamepata nafasi ya kuwa nao kwa muda mrefu na kutambua maendeleo yao.
  Nahodha wa kikosi cha Bara, John Bocco ataongoza timu kwenye michuano ya Challenge nchini Ethiopia 

  “Tumechagua wachezaji kulingana na mahitaji ya timu, tumekua na wachezaji hawa kwa muda mrefu katika vipindi mbalimbali, tuna amini tuliowachagua watafanya vizuri katika michuano hiyo mikongwe barani Afrika” amesema Kibadeni.
  Wachezaji walioitwa ni makipa, Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam), Said Mohamed (Mtibwa Sugar). Mabeki Shomari Kapombe (Azam), Hassan Kessy (Simba), Mohammed 'Tshabalala' Hussein (Simba), Hassan Isihaka (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa), Juma Abdul (Yanga) na Kelvin Yondani (Yanga).
  Viungo Himid Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Said Ndemla (Simba), Salum Telela (Yanga), Salum Abubakar (Azam), Deus Kaseke (Yanga), washambuliaji John Bocco (Azam), Elias Maguri (Stand United), Ibrahim Hajibu (Simba), Malimi Busungu (Yanga) na Saimon Msuva (Yanga).
  Michuano ya Kombe la Chalenji inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 21 na kumalizika Disemba 6, ambapo Kilimanjaro Stars imepangwa kundi A, lenye wenyeji Ethiopia, Rwanda na Somalia.
  Wachezaji Said Mohamed, Juma Abdul, Hassan Kessy, Hassan Isihaka, Salum Abubakar na Ibrahim wanaendelea na mazoezi jijini Dar es salaam chini ya kocha msaidizi Juma Mgunda wakati wanawasubiri wachezaji wengine walioko nchini Algeria na kikosi cha Taifa Stars.Kundi B lina Bingwa Mtetezi Kenya, Burundi, Uganda na Zanzibar, huku kundi C likiundwa na timu za Sudan, Sudani Kusini, Djibouti na waalikwa wa michuano hiyo timu ya taifa kutoka Malawi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: 'KING KIBADENI' ATAJA KIKOSI CHA UBINGWA CHALLNGE 2016 ADDIS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top