• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 26, 2015

  AMISSI TAMBWE AWATUNGUA WAKENYA, ETHIOPIA YAWAFUNGA 2-0 SOMALIA

  Mshambuliaji wa Yanga SC, Amissi Tambwe amwfunga bao jana Challenge
  KENYA imelazimisha sare ya 1-1 na Burundi katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki ya Kati, CECAFA Challenge Jumatano nchini Ethiopia.
  Mshambuliaji wa Yanga SC, Amissi Tambwe alianza kuifungia Burundi dakika ya 11 kabla ya mpachika mabao wa Gor Mahia, Michael Olunga kuisawazishia Kenya dakika ya 41.
  Mchezo wa Kundi A, wenyeji Ethiopia wameshinda 2-0 dhidi ya Somalia mabao ya Mohammed Nasser na Behailu Girma.
  Mechi za Kundi C, Malawi imeichapa mabao 3-0 Djibouti, mabao ya Gerlad Phiri Jnr, John Banda na Chiukepo Msowoya wakati Sudan Kusini imetoka sare ya 0-0 na Sudan.
  Leo ni mapumziko na kesho mechi za makundi zinatarajiwa kuhitimishwa kwa mechi kati ya Rwanda Vs Somalia, Zanzibar Vs Kenya, Sudan Kusini Vs Malawi, Djibouti Vs Sudan, Uganda Vs Burundi na Tanzania Vs Ethiopia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AMISSI TAMBWE AWATUNGUA WAKENYA, ETHIOPIA YAWAFUNGA 2-0 SOMALIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top