• HABARI MPYA

  Jumanne, Novemba 17, 2015

  ULIMWENGU AUMIA GOTI MAZOEZINI, SASA HATARINI KUWAKOSA ALGERIA LEO

  Na Mahmoud Zubeiry, BLIDA
  MSHAMBULIAJI Thomas Emmanuel Ulimwengu yuko kenye hatihati ya kuichezea Tanzania dhidi ya wenyeji Algeria mchezo wa marudiano Raundi ya Pili kufuzu Kombe la Dunia usiku wa leo.
  Hiyo inafuatia kuumia goti usiku wa jana katika mazoezi baada ya kugongana na kiungo Said Hamisi Ndemla Uwanja wa Mustapha Tchaker mjini Blida.
  Ulimwengu anayechezea klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) aliumia baada ya dakika 30 tu na kushindwa kuendelea na mazoezi.
  Madaktari wa Taifa Stars, wakiongozwa Dk Richard Yomba walijaribu kumpatia huduma ya kwanza, lakini haikuweza kumpa ahueni ya kuendelea na mazoezi.
  Thomas Ulimwengu ameumia mazoezini jana usiku na huenda asicheze leo

  Dk Yomba ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo asubuhi kwamba watamfanyia uchunguzi Ulimwengu baadaye leo kujua maendeleo ya maumivu yake.
  “Tutamfanyia uchunguzi baadaye kujua maendeleo yake kama atakuwa kwenye nafasi ya kucheza au, la”amesema Dk Yomba.
  Taifa Stars inatarajiwa kushuka kwenye Uwanja Mustapha Tchaker mjini Blida kuanzia Saa 1:15 usiku na Saa 3:15 Usiku kwa Saa za nyumbani, Tanzania.
  Stars itahitaji kulazimisha ushindi wa ugenini, ili kusonga hatua ya mwisho ya mchujo wa mbio za Urusi 2018 baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 katika mchezo wa kwanza Jumamosi, Dar es Salaam. 
  Kocha Mkuu wa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema wachezaji wake wana morali kubwa kuelekea mchezo huo na hali ya hewa ya baridi haiwezi kuwa kikwazo kwao.
  “Baada ya mazoezi ya leo (jana) vijana wako vizuri na ninaamini watafanya vizuri kutokana na morali waliyokuwa nayo ya kimchezo,”amesema. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ULIMWENGU AUMIA GOTI MAZOEZINI, SASA HATARINI KUWAKOSA ALGERIA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top