• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 29, 2015

  WLADIMIR KLITSCHKO KWISHA HABARI YAKE, ADUNDWA NA TYSON FURY HADI HURUMA!

  BONDIA Tyson Fury ndiye bingwa mpya wa ndondi za kulipwa uzito wa juu, baada ya kumdunda Wladimir Klitschko katika pambano kali la kihistoria.
  Muingereza Tyson Fury amemshinda Wladimir Klitschko wa Ukraine kwa pointi usiku wa jana mjini Dusseldorf, Ujerumani na kijana huyo wa umri wa miaka 27 anabeba mataji yote makubwa ya ngumi uzito wa juu, WBA, IBF na WBO.
  Fury hakumpa nafasi Klitschko ya kufurukuta ulingoni kutokana na kumsukumia makonde mfululizo akitumia mikono na mitindo yote kiasi cha 'kumharibu sura' mpinzani wake huyo aliyekuwa mbabe wa ndondi za uzito wa juu kwa karibhu muongo wote huu.
  Baada ya kumdunda mbabe wa muda mrefu wa ndondi za uzito wa juu, Wladimir mwenye umri wa miaka 39, sasa Fury anatarajia kupambana na Mmarekani, Deontay Wilder anayeshikilia taji la WBC.

  Klitschko akivuja damu kutokana na kipigo cha jana kutoka kwa Tyson Fury PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WLADIMIR KLITSCHKO KWISHA HABARI YAKE, ADUNDWA NA TYSON FURY HADI HURUMA! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top