• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 27, 2015

  KING KIBADEN: TUTACHEZA KWA TAHADHARI KUHIFADHI NGUVU KWA AJILI YA ROBO FAINALI

  RATIBA KOMBE LA CHALLENGE 2015
  Leo; Novemba 27, 2015
  Rwanda Vs Somalia
  Zanzibar Vs Kenya
  S. Sudan v Malawi
  Djibouti V Sudan
  Kesho; Novemba 27, 2015
  Uganda Vs Burundi 
  Tanzania Vs Ethiopia
  King Kibaden amesema leo watacheza kwa tahadhari nguvu zao kwa ajili ya Robo Fainali 

  Na Mwandishi Wetu, ADDIS ABABA
  KOCHA Mkuu wa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ amesema kwamba leo watacheza kwa tahadhari ili kutunza nguvu zao kwa ajili ya Robo Fainali.
  Kili Stars inamenyana na wenyeji, Ethiopia kesho katika mchezo wa mwisho wa Kundi A michuao ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mjini Addis Ababa, Ethiopia.
  Na Kibadeni amesema watapigania ushindi, lakini hawatatumia nguvu nyingi kukwepa kujichosha na wachezaji kuumia, wakati timu imekwishatinga Robo Fainali.
  “Tunajua wenzetu wanataka sana ushindi ili waende Robo Fainali. Na kwa sababu ni wenyeji, tunatarajia hata marefa watakuwa upande wao. Tutajaribu kupambana tusipoteze mchezo. Hilo ndilo kubwa,”amesema Kibadeni.
  Kwa ujumla mshambuliaji huyo wa zamani wa kimataifa nchini, amesema wachezaji wake wako vizuri kuelekea mchezo wa jioni ya leo na ana matumaini ya ushindi.
  Kili Stars imejihakikishia Robo Fainali baada ya ushindi mfululizo katika mechi mbili za awali, 4-0 dhidi ya Somalia na 2-1 dhidi ya Rwanda na leo inakamilisha mechi zake za Kundi A ikiwa kileleni. 
  Mechi za makundi za Challenge 2015 zinahitimishwa leo Rwanda ikimenyana na Somalia, Zanzibar na Kenya, Sudan Kusini na Malawi, Djibouti na Sudan, wakati kesho Uganda itamenyana na Burundi na Tanzania na Ethiopia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KING KIBADEN: TUTACHEZA KWA TAHADHARI KUHIFADHI NGUVU KWA AJILI YA ROBO FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top