• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 16, 2015

  ‘NGONGOTI’ WA SIMBA ACHEMSHA MBIO ZA KERR MLIMANI, RAUNDI MBILI TU ‘AOMBA POO’

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI Msenegali wa Simba SC Pape Abdoulaye N’daw leo asubuhi ameshindwa mazoezi ya kukimbia Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
  Simba SC imeanza mazoezi leo asubuhi baada ya mapumziko ya wiki mbili, kujiandaa na mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC mwezi ujao.
  Wachezaji 11 wamejitokeza mazoezini Simba SC leo kutokana na wengine kuwa kwenye timu zao za taifa kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
  Pape Abdoulaye N'daw leo ameshindwa mazoezi ya kukimbia Chuo Kikuu

  Na Kocha Muingereza, Dylan Kerr ambaye sasa anafanya kazi peke yake baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Msaidizi wake, Suleiman Matola leo aliwapa wachezaji mazoezi ya kukimbia.
  Waliojitokeza mazoezini leo ni makipa Vincent Angban na Peter Manyika, Nahodha Mussa Mgosi, N’daw, Joseph Kimwaga, Said Issa na Issa Abdallah.
  Hata hivyo, N’daw aliyesajiliwa msimu huu alikimbia raundi tatu kabla ya kuchoka na kushindwa kuendelea kukimbia katika raundi ya nne kati ya 10 alizowapa Kerr.
  Mchezaji huyo mrefu kuliko wote wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara alisababisha wachezaji wenzake wamcheke baada ya kushindwa kuendelea kukimbia kuuzunguka Uwanja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ‘NGONGOTI’ WA SIMBA ACHEMSHA MBIO ZA KERR MLIMANI, RAUNDI MBILI TU ‘AOMBA POO’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top