• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 23, 2015

  BENZEMA PEKEE ALIIBUKA MAZOEZINI REAL JANA BAADA YA 4-0 ZA BARCA JUZI

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ufaransa, Karim Benzema jana alikuwa mchezaji pekee aliyecheza timu hiyo ikifungwa 4-0 na Barcelona Uwanja wa Santiago Bernabe katika La Liga kuripoti mazoezini.
  Mfaransa huyo aliibuka mazoezini viwanja vya Valdebebas kuungana na wachezaji ambao hawakucheza El Clasico Jumamosi akina Casemiro, Alvaro Arbeloa and na Lucas Vazquez.

  Benzema na nyota wenzake wa Real, Gareth Bale na Cristiano Ronaldo walishindwa kutikisa nyavu za Barca mara moja juzi. PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Luisa Suarez alifunga mabao mawili katika ushindi huo, wakati Neymar na Andres Iniesta kila mmoja alifunga bao moja, Real ikipoteza mechi ya kwanza ya La Liga nyumbani baada ya mechi 23. 
  Kikosi kizima cha Real kinatarajiwa kufanya mazoezi kamili leo kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Shakhtar Donetsk
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BENZEMA PEKEE ALIIBUKA MAZOEZINI REAL JANA BAADA YA 4-0 ZA BARCA JUZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top