• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 21, 2015

  CECAFA YAPATA RAIS MPYA, DK JAFFER ARITHI KITI TENGA

  Tenga kulia akimkaribisha Dk. Jaffer
  MSUDANI Dk. Mutasim Jaffer amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati, CECAFA jana akichukua nafasi ya Mtanzania, Injinia Leodegar Tenga.
  Mutasim amepata kura sita kati ya 10 dhidi ya wapinzani wake, Mganda Lawrence Mulindwa aliyeoata kura tatu na Vincent Nzamwita wa Rwanda aliyeambulia kura moja, wakati Junedin Basha wa Ethiopia alijitoa kwenye uchaguzi huo dakika za mwishoni.
  Katika hotuba yake ya kumkaribisha Rais mpya, Tenga alisema Jaffer ni mtu anayefaa kuongoza CECAFA.
  "Nina furaha kukabidhi madaraka kwa mtu ambaye ni mweledi na anapenda soka. Tunataka kuona CECAFA inakuwa katika michache ijayo na kunufaika na programu mpya za maendeleo za FIFA,"amesema Tenga.
  "Nina furaha nimefanya mazuri katika miaka yangu minane iliyopita kama Rais, lakini nitakuwa tayari wakati wowote kwa ushauri nikihitajika,” amesema Tenga.
  Kwa upande wake, Rais mpya wa CECAFA, Jaffer amesema kwamba anatarajia kuinua kiwango cha soka ya ukanda huu kimataifa.
  "Uchaguzi huu hauna mshindi wala washindwa, naamini sisi ni familia moja na ninataka haraka kuingia kazini kubadiliosha mwonekano wa soka ya nchi wanachama za CECAFA na kuhakikisha tunayapatia udhamini mashindano yote, kuanzia ya vijana chini ya umri wa miaka 17 hadi ya wakubwa,"amesema.
  Uchaguzi wa CECAFA umefanyika Addis Ababa, Erhiopia jana ambako leo michuano ya Kombe la Challenge inaanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CECAFA YAPATA RAIS MPYA, DK JAFFER ARITHI KITI TENGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top