• HABARI MPYA

  Jumamosi, Novemba 28, 2015

  NI VITA YA USUKANI LIGI KUU ENGLAND LEO, MAN UNITED WAWAFUATA VINARA LEICESTER

  RATIBA LIGI KUU YA ENGLAND WIKIENDI HII
  Leo Jumamosi; Novemba 28, 2015
  Sunderland Vs Stoke City (Saa 12:00 jioni)
  Manchester City Vs Southampton (Saa 12:00 jioni) 
  Crystal Palace Vs Newcastle Utd (Saa 12:00 jioni)
  Bournemouth Vs Everton (Saa 12:00 jioni)
  Aston Villa Vs Watford(Saa 12:00 jioni)
  Leicester City Vs Manchester Utd (Saa 2:00 usiku)
  Kesho Jumap[ili; Novemba 29, 2015
  Tottenham Hotspur Vs Chelsea (Saa 9:00 Alasiri)
  West Ham United Vs West Brom (Saa 11:00 jioni)
  Norwich City Vs Arsenal (Saa 1:15 usiku)
  Liverpool Vs Swansea City (Saa 1:15 usiku)  
  Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney ataiongoza timu katika vita muhimu leo

  KOCHA Louis Van Gaal anasafiri na skwadi lake la Manchester United hadi Uwanja wa King Power kuwafuata vinara wa Ligi Kuu ya England, Leicester City mchezo utakaoanza Saa 1:30 usiku.
  Leicester wenye pointi 28, wanaizidi pointi moja Man United kileleni baada ya timu zote kucheza mechi 13 na mshindi wa leo ataongoza Ligi Kuu kwa wastani mzuri kidogo wa pointi.
  Nahodha wa United, Wayne Rooney anafahamu makali ya mkali wa mabao wa Leicester, Jamie Vardy kuelekea mchezo wa leo na ametahadharidha.
  Mshambuliaji huyo wa Leicester, Vardy ataweka historia Uwanja wa King Power iwapo atafunga kwa amra ya 11 mfululizo katika Ligi Kuu.
  Akiwa amefunga mabao 13 katika Ligi Kuu hadi sasa, Vardy amefunga mabao mengi kuliko safu yote ya ushambuliaji ya United – na atavunja rekodi ya gwiji wa Old Trafford, Mholanzi Ruud van Nistelrooy iwapo atafunga leo.

  Mshambuliaji wa Leicester City, Jamie Vardy anawania kuvunja rekodi ya Ruud van Nistelrooy kwa kuvunja mara 11 mfululizo katika Ligi Kuu ya England

  Rooney na washambuliaji wenzake wa United kwa pamoja wamefunga mabao tisa tu na katikati ya wiki walishindwa kufunga timu ikilazimishwa sare ya 0-0 na PSV Eindhoven katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Kwa ujumla Ligi Kuu ya England inaendelea leo, Sunderland wakiikaribisha Stoke City, Manchester City na Southampton, Crystal Palace na Newcastle United, Bournemouth na Everton na Aston Villa na Watford, wakati kesho Tottenham Hotspur watakuwa wenyeji wa Chelsea, West Ham United na West Bromwich Albion, Norwich City na Arsenal na Liverpool na Swansea City.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI VITA YA USUKANI LIGI KUU ENGLAND LEO, MAN UNITED WAWAFUATA VINARA LEICESTER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top